Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akitembelea mabanda katika Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024) lililoanza leo Disemba 2, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza jambo katika ufunguzi Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024) lililoanza leo Disemba 2, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza jambo katika ufunguzi Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024) lililoanza leo Disemba 2, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu akizungumza jambo katika ufunguzi Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024) lililoanza leo Disemba 2, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akiwametunukiwa vyeti waafiti kwa kutambua mchango wao kwa maendeleo yaliyofikiwa katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, kilimo na uvuvi.
……………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2021-2024 imetoa zaidi ya shilingi bilioni 32 kwa ajili ya kuimarisha miradi ya wanasayansi ya kufanya utafiti na ubunifu katika sekta zaidi ya 20 ikiwemo kilimo, elimu, Afya pamoja na nishati.
Akizungumza leo Disemba 2, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akimwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa serikali inatambua mchango wa wanasayansi na kuwawezesha watafiti na wabunifu.
Dkt. Biteko amesema kuwa serikali itaendelea kuthamini mchango wa wanasayansi kwa Taifa kupitia tafiti zao, huku akisisitiza umuhimu wa kupanua wigo ili tafiti hizo zijibu changamoto za kiuchumi.
“Wanasayansi wanafanya kazi nzuri na kubwa ya kutafuta suluhu ya matatizo mbalimbali katika jamii, lakini kazi zao zinatambuliwa zaidi nje ya nchi kuliko zinavyotambuliwa hapa nchini jambo ambalo linaweza kuwavunja moyo” amesema Dkt. Biteko.
Amesema kuwa wakati umefika kwa serikali na mashirika kutambua, kuthamini na kutumia tafiti za wanasayansi wa ndani ya nchi ili kutatua changamoto zilizopo.
Dkt. Biteko amesema kuwa kongamano hilo litumike kujadili na kutafuta suluhu ya matatizo yaliyopo nchini, huku akieleza umuhimu wa kila aliyejaribu kufanya tafiti apewe fursa ya kuendeleza utafiti wake.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda, amesema kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa mikopo nafuu wa kubiasharisha bunifu na tafiti Tanzania unaojulikana kama Samia Fund.
“Serikali inatambua jitihada za wanasayansi, watafiti wa ndani ya nchi na baadhi yao wametunukiwa vyeti kwa kutambua mchango kwa maendeleo yaliyofikiwa katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, kilimo na uvuvi” amesema Profesa Mkenda.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu, amesema kuwa kupitia program mbalimbali wa wameweza kuwasaidia vijana kubadili maisha yao kwa kupata fursa, huku akifafanua kuwa wamefanikiwa kutoa vibali 1, 000 kwa watafiti kutoka nje ya nchi.
Amesema kuwa zaidi ya Taasisi 140 za utafiti nchini zimefungamana na COSTECH ikiwa ni juhudi za kukuza na kusimamia maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini.
“Sera ya Serikali ni kuwezesha na kuifungua nchi, kushirikiana na nchi mbalimbali katika kufanya tafiti pamoja na kuendeleza ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kubadilishana uzoefu” Dkt. Nungu.
Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na Maonesho (STICE 2024) Dkt. Biteko amezindua Mfuko wa mikopo nafuu ‘SAMIA FUND’ , kongamano hilo litafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Disemba 2, 2024 ambalo limebeba kauli mbiu isemayo: Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika kuimili changamoto za mabadiliko ya Tabia ya Nchi na kuchangia katika uchumi shindani.