Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Disemba 02, 2024 akisaini Kitabu cha Maombolezo kwenye msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Disemba 2, 2024 ameshiriki Misa ya kuaga mwili wa Ndugulile iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam.
Katika misa hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Dkt. Ndugulile na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Shirikisho la Mabunge Duniani (IPU).
Dk. Faustine Ndugulile, Alikuwa ameteuliwa kushika nafasi hiyo Agosti 27, 2024, na alitarajiwa kuanza rasmi majukumu yake mwaka 2025.
Mazishi yake yatarajiwa kufanyika Kigamboni, Dar es Salaam, mnamo Desemba 3, 2024.