Mtangamano kwa maslahi mapana ya wananchi wao.
Mkutano huo ambao ulitanguliwa na Mikutano ya Kamati ya Wataalam uliofuatiwa na Kamati ya Uratibu ya Makatibu
Wakuu na Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo, pamoja na mambo mengine umemteua Rais wa Kenya, Mhe. William Ruto kuwa
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Novemba 2024
hadi Novemba 2025 akisaidiana na Rais wa
Somalia, Mhe. Hassan Sheikh Mohamud.
Aidha, Mkutano huo mbali na kuridhia
Lugha za Kiswahili na Kifaransa kuwa Lugha rasmi za EAC zikienda sambamba na
Kiingereza pia umezitaka nchi wanachama za Tanzania, Rwanda, Sudan Kusini,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Somalia kukamilisha mashauriano ya kitaifa
kuhusu katiba ya shirikisho la kisiasa la EAC ifikapo Juni 30, 2025.
Vilevile, Wakuu hao wa Nchi wameridhia utezi wa Jaji Richard
Wejuli Wabwire kutoka Uganda kuwa Naibu Jaji Mkuu wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki kuanzia
mwezi Novemba 2024.
Katika hatua nyingine, wakuu hao wa nchi waliwapongeza
wananchi wote wa Nchi wanachama wa EAC kwa kuadhimisha miaka 25 ya Mtangamano
wa Kikandana kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika biashara, kudumisha
amani na usalama, kuwawezesha wanawake
na vijana kiuchumi, kuzalisha bidhaa kibiashara na kulinda mazingira kwa
kuhamasisha matumizi ya nishati safi na kuzingatia mageuzi ya kidigiti kama
kichocheo muhimu katika kukuza Mtangamano.
Akizungumza, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye pia ni Mwenyeji wa Mkutano huo,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema kuwa Tanzania itaendelea kuunga
mkono agenda ya Mtangamano wa Kikanda wa EAC kwani Tanzania inaamini katika
Umoja kuliko utengano.
Amesema EAC inasherehekea kutimiza miaka 25, Tanzania
itaendelea kuenzi maono ya viongozi waanzilishi wa EAC akiwemo Hayati Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuhakikisha umoja na undugu
unaoziunganisha nchi hizi unadumishwa kwa
maslahi ya wananchi wan chi hizo.
Tangu tupate uhuru hadi Muungano neno Umoja ni
tunu hapa Tanzania. Hivyo tutaendelea kudumiasha umoja wetu katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki ili kuwaenzi waanzilishi wa maono haya akiwemo Hayati Mwalimu
Nyerere”, alisema Mhe. Rais Samia.
Pia alimpongeza Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri
Museveni ambaye naye ni mwanzilishi wa Jumuiya hiyo kwa kuendelea kusimamia
misingi ya umoja, amani na mshikamano katika Jumuiya ambapo pia alimtakia afya
njema na maisha marefu.
“Tunamshukuru Rais Museveni ambaye amekuwa Mwalimu
kwetu, msuluhishi na kwa kifupi tunamwita Dean yaani kiongozi wetu katika
Jumuiya ambapo kila tunapotaka kuengeuka anaturejesha” alisisitiza Rais Samia.
Mbali na Mhe. Rais Samia, Mhe. Rais Ruto na Mhe.
Rais Mohamud, Mkutano huo pia ulimshirikisha Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta
Museveni, Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame na Makamu wa Rais wa Burundi Mhe.
Prosper Bazombaza.
Aidha, Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Mhe. Veronica Nduva
ambaye alishiriki kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake kwenye wadhifa huo.
Viongozi wengine walioshiriki ni Mawaziri kutoka
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Fedha,
Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji,
Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na
Uwekezaji-Zanzibar, Mhe. Shariff Ali Shariff, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.
Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Selemani Jafo na
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda-Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaaban.
Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi wa EAC uliofanyika jijini Arusha tarehe 30 Novemba 2024 |
Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa wamesimama kama ishara ya heshima wakati wimbo wa Taifa la Tanzania kama mwenyeji wa mkutano na wibo wa Afrika Mashariki zikiimbwa |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC uliofanyika jijini Arusha Novemba 30, 2024 |
Wageni waalikwa wakati wa Mkutano |