Simba SC imefanikiwa kuanza vizuri Mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya makundi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravos do Maquis katika mchezo uliochezwa leo Novemba 27, 2024 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
Bao la Simba SC limefungwa na Kiungo chipukizi Jean Charles Ahoua kwa mkwaju wa penalty dakika ya 27 ya mchezo.
Simba SC itakuwa na mchezo mmoja wa Ligi Kuu NBC Tanzania Bara dhidi ya Singida Black Starts ugenini Disemba 1, 2024 kabla ya kusafiri kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa pili wa Kundi A Kombe la Shirikisho utakaopigwa Disemba 8, 2024 katika Uwanja wa Mohamed Hamlaou mjini Constantine.