Mteja wa Vodacom Tanzania Plc, Regina Mbalamwezi akirudishiwa nauli yake baada ya kukata tiketi ya basi kupitia M-Pesa kutoka Dar es Salaam Kwenda Morogoro wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa’ katika kituo cha mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Biashara kutoka Vodacom Tanzania, Brigita Shirima akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kampuni hiyo ya ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa!’ lenye lengo la kuhamasisha wateja wake kufanya miamala yao kutumia M-Pesa wakati wa msimu huu wa sikukuu. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni.
Timu kutoka Vodacom Tanzania Plc wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa!’ tarehe 26 Novemba 2024 jijini Dar es Salaam kuhamasisha wateja wa Vodacom kutumia kufanya malipo kutumia M-Pesa ambapo wanajiweka kwenye nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwamo wateja 1,500 kurudishiwa nauli za mabasi, tiketi 100 za bure za SGR pamoja na punguzo za aina mbalimbali katika miamala yao.
Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Biashara kutoka Vodacom Tanzania, Brigita Shirima (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa ‘Shangwe Popote Ukitumia M-Pesa’ uliofanyika kituo cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Uzinduzi wa kampeni kabambe ya ‘Shangwe Popote Ukilipa Kwa M-Pesa’ ambayo inahamasisha wateja wa Vodacom kufanya miamala kupitia M-Pesa’