Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mkoa wa Ruvuma Mhe. Jenista Mhagama leo Novemba 27, 2024 ameungana na wananchi wa kitongoji cha Magigi, kata ya Parangu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuchagua vongozi kwa nafasi za Mwenyekiti wa Kijiji, Kitongoji, Mjumbe wa Kundi Mchanganyiko na Mjumbe wa Kundi la Wanawake. Ametoa shime kwa wananchi wa maeneo mengine kujitokeza kwenye uchaguzi huu kuchagua viongozi ngazi ya msingi watakaosaidiana nao bega kwa bega kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.