Na Oscar Assenga,MUHEZA.
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ametoa siku saba kwa mkandarasi anayejenga mradi wa Maji wa Miji 28 kwa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kuanza ujenzi wa tenki katika eneo la Kilulu kutokana na ujenzi wake kutokuanza tofauti na ilivyo kwa wilaya nyengine zinazotekeleza mradi huo.
Aweso alitoa agizo hilo wakati wa muendelezo wa muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji hasa ile miji 28 inayoendelea mkoani Tanga ambapo akiwa wilayani Muheza kwenye mradi wa Kilulu alieleza na Mkuu wa wilaya hiyo Zainabu Abdallah kwamba mpaka sasa mkandarasi amechimba mashimo na hatuna kinachoendelea.
Kutokana na taarifa hiyo Waziri huyo alilazimika kutoa maelekezo hayo kwa mkandarasi huyo kuhakikisha pia wanafanya kazi Kwa ufanisi ili uweze kukamilika na wananchi waweze kupata huduma ya maji
Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainabu Abdallah alimuomba Waziri Aweso kumchukulia hatua za mkandarasi huyo kutokana na mpaka sasa kuchimba mashimo tu na hakuna hatua yoyote inayoendelea .
“Mh Waziri tunashuku Kwa ziara hii na tunaamini ujio wako utakuwa faraja Kwa wananchi kwani utawasaidia kuusukuma mradi ufanye kazi kwa haraka na wananchi wapate maji”Alisema
Awali akizungumza kwa upande wake Mwenyekit wa Halmashari ya Muheza Erasto Mhina alisema Baraza la Madiwani walikaa na kujadili suala hilo na mbunge ila hata walipotoa agizo bado hakuna kilichoendelea mpaka sasa hivyo kumuomba waziri achukua hatua ili ujenzi wake uanze.
Naye Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa wilaya ya Muheza Cleophace Maharangata wakandarasi hao amekiri kutokuridhishwa na ujenzi wa matenki hayo na hivyo kuhaidia mbele ya Waziri kwamba watahakikisha wanaisimamia ujenzi huo kwa ukaribu zaidi.
Mradi wa Miji 28 wa HTM kwa mkoa wa Tanga unahusisha wilaya ya Handeni,Muheza,Pangani na Korogwe ambapo utagharimu kiasi cha sh Bilioni 170 hadi kukamilika kwake kwa hatua za awali.