Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 19, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania, kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo unawakutanisha wadau wa madini wanaojishughulisha na utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani madini, wasimamizi wa Sekta kutoka Serikalini, watoa huduma migodini na wafanyabiashara.
Pamoja na malengo mengine, mkutano huo umelenga kuweka mipango ya kuvutia uwekezaji wa nje ya nchi, kukuza usimamizi bora wa rasilimali za Madini pamoja na kubadilishana uzoefu na washiriki kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Uongezaji wa Thamani ya Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi”