Na Prisca Libaga Arusha
SERIKALI imewataka Wasimamizi na maafisa rasilimali watu wa Sekta ya Umma na binafsi barani Afrika wazingatie swala la Utawala bora, utumishi wa umma wenye tija katika kusimamia rasilimali watu ili kutoa huduma bora na kudumisha Imani ya Wananchi kwa Serikali zao barani Afrika.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Katiba,Sheria Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Haroun Ally Suleiman alipokuwa akifunga kongamano la 9 la Wasimamizi na maafisa raslimali watu barani Afrika kwenye Ukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC, Jijini Arusha.
Amesema lengo la kongamano hilo la siku tatu lilikuwa ni kuwawezesha wasimamizi na maafisa rasilimali watu hao kutoka nchi wanachama kubadilisha uzoefu, kujifunza na kupata uelewa mpana na mwelekeo wa kidunia katika usimamizi wa raslimali watu na maendeleo makubwa ya kiteknolojia yanayoshuhudiwa kupitia mawasiliano.
Amesema Wasimamizi na maafisa rasilimali watu Wamejengewa uwezo katika maswala mbalimbali kupitia mada 29 hivyo watazisaidia Serikali zao kwenye maeneo muhimu waliyojengea uwezo kuhusua usimamizi raslimali watu Utawala imara,ubunifu na usimamizi wa hifadhi na kwa ajira endelevu zenye ushindani na mchakato wa ajira kwenye njia ya kidigitali katika Utumishi wa umma
Waziri Haroun amesema kuwa uwezo waliojengewa kuhusu mpango wa uwezeshaji, madaraka, uwajibikaji na uwazi katika Utumishi wa umma na maswala ya usimamizi wa rasilimali watu katika kukuza usimamizi utoaji huduma kupitia ushirikiano wa Sekta ya umma na binafsi utawezesha kutolewa huduma bora na kwa wakati.
Amesema kongamano hilo lenye kauli mbiu isemayo Utawala stahilivu na ubunifu kukuza Sekta ya umma ijayo kupitia uongozi wa raslimali watu limekuwa na mafanikio makubwa Kwa kuwa limeshirikisha Wasimizi na mameneja rasilimali watu katika Sekta ya umma na binafsi barani afriika
Amesema kuwa washiriki hao wamepata fursa ya kujadili changamoto wanazokutana nazo na namna ya kuzitatua akasisitiza Uongozi uendelee kuhamasisha usitawi wa Jumuiya hiyo barani Afrika uwepo uwakilishi mzuri kila kanda Kwa kutambua kwamba raslimali watu ndio uti wa mgongo wa taasisi za nchi zetu kwa Jumla
Amesisitiza waajiri kugharimia maafisa raslimali kuhudhuria makingamano Ili wawe wabunifu watoe huduma bora na akawataka Wasiamizi na waajiri wahakikishe watumishi wanapata stahiki zao kwa wakati iwe ni motisha wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Magmenti ya Utumishi wa Umma,Zena Saidy amesema kongamano hilo la siku tatu ni muhimu sana kwa mstakabali wa maendeleo ya raslimali watu katika nchi zetu majadiliano hayo yatasaidia kwenda kuboresha raslimali watu .
Ameshauri ziwepo fomu za kufanya tathimini na kutoa mapendekezo kwa kuwa zitasaidia kuboresha utendaji na utolewaji huduma.
Amesema mameneja rasilimali watu wanatakiwa wawe ni waelewa wao ni kimbilio la watumishi wanapokuwa wamekwazika katika maeneo yao ya kazi wawasikilize na kutatua changamoto zao .
Zena, amewataka watumie teknolojia katika kurahisisha mifumo katika nchi zetu kwa kuwa mifumo inasaidia kurahisisha maswala ya Utumishi wa umma,na Tanzania imepata tuzo kwenye mifumo ya e- mrejesho ,kutoka kwa Wananchi kutokana na huduma wanazozitoa kwa umma.
Amesema kuwa Zanzibar wanao mfumo wa sema na rais,ambao huduma zinazotolewa na Serikali kwa Wananchi umesaidia sana upatijanaji wa huduma kwa haraka na wanaokiuka wanachukuliwa hatua.