Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kulia) akizungumza jambo na Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi. Katikati ni Makamu wa Rais wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) Bw. James Wasagami.
Mawaziri na Viongozi mbalimbali kutoka Bara la Afrika (meza kuu) wakitoa uzoefu wao kuhusu usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakati wa Mkutano wa 9 wa Mwaka wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (Wa kwanza kulia) akifuatilia Mkutano wa 9 wa Mwaka wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Bw. Omar Gora.
Mawaziri na Viongozi mbalimbali kutoka Bara la Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa uzoefu wao kuhusu usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakati wa Mkutano wa 9 wa Mwaka wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Mtumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Vincent Ngure akielezea mifumo ya kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya utumishi wa umma kwa baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 9 wa Mwaka wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).
Baadhi ya wajumbe wa sekretarieti ya maandalizi ya Mkutano wa 9 wa Mwaka wa Mtandao wa Mameneja Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Afrika (APS-HRMnet) wakiwa katika picha ya pamoja katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).