Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewaagiza wasimamizi wa uchaguzi Mkoa wa Iringa, kuhakikisha Uchaguzi wa Mwaka huu unasimamiwa vizuri na unakuwa wa Uhuru na haki.
Ameyasema hayo leo Novemba 05,2024 wakati alipokutana na viongozi Mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya, wakuu wa idara Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Maafisa Tarafa na waratibu wa uchaguzi kutoka katika kila Halmashauri.
Mhe. Serukamba amesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa uchaguzi wa kipekee tofauti na chaguzi zingine hivyo amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha kila jambo linalofanyika vyama vyote viweze kushilikishwa kuanzia ujazaji wa fomu maandalizi ya vituo na kazi zingine vyama viwezwe kushirikishwa katika kila hatua inayofanyika
Pia ameongeza kwa kusema kuwa Zimetolewa siku chache kwaajili ya kuongeza vituo vya kupigia kura hivyo wakurugenzi na waratibu wa uchaguzi wahakikishe wanasimamia na kushirikisha vyama vingine katika kupendekeza sehemu za kuongeza vituo ili wananchi wasitembee umbali mrefu kwenda kupiga kura.
Aidha Mhe. Seeukamba amewapongeza waratibu wote wa uchaguzi mkoani Iringa kwa kazi nzuri walioifanya katika kuwahimiza wananchi kujitokeza katika kujiandikisha kwenye daftari la mkazi.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajia kufanyika Novemba 27,2024 nchi nzima.