Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kulia) akikabidhi mifuko 20 ya saruji kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Mnyigumba Bw. Richius Mwamanga (wa nne kulia) kwa lengo la kuunga mkono juhudi za wananchi katika ujenzi wa jiko la Shule hiyo mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikoroga uji kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Myigumba iliyopo mkoani Iringa wakati wa ziara yake Shuleni hapo kuangalia masuala ya Lishe.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akichimba shimo katika shamba la Shule ya Msingi Mnyigumba iliyopo Rungemba mkoani Iringa kwaajili ya kushirikiana na wananchi kupata mahindi shambani wakati wa ziara yake Shuleni hapo kuangalia masuala ya Lishe.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipanda mbegu ya mahindi katika shamba la Shule ya Msingi Mnyigumba iliyopo Rungemba mkoani Iringa wakati wa ziara yake Shuleni hapo kuangalia masuala ya Lishe.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
*********************************
Na Mwandishi Wetu Iringa
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuweke mkazo kwa kutoa elimu ya lishe nchini hasa katika shule za misingi na Sekondari nchini ili kuondokana na tatizo la udumavu na utapiamlo.
Ameyasema hayo leo mkoani Iringa alipotembela Shule ya msingi Mnyigumba ambapo shule hiyo imelima shamba kwa ajli ya mahindi lishe yatakayosaidia kuwapatia mlo wa asubuhi na mchana wanafunzi.
Ameongeza kuwa Sera ya elimu bure ina maana ya kuwa wazazi na walezi kutochangia katika kuhakikisha wananfunzi wanapata chakula wakati wakiwa shleni ili kuhakikisha wanazingatia masomo yao na kuongeza ufaulu.
“Elimu bure sio sababu ya wazazi, walimu na shule kutokuwa wabunifu katika kuhakikisha wanajiongeza katika masuala ambayo yatasaidia wanafunzi kuongeza juhudi katika masomo na kuongeza ufaulu”alisema Dkt. Ndugulile.
Amesisitiza kuwa elimu ya lishe inatakiwa kutolewa kwa wananchi hasa katika maeneo ambayo tatizo la udumavu na utapiamlo linaongezeka kwa kasi katika maeneo ya Nyanda za juu kusini ikiwemo mkoa wa Iringa ingawa mikoa hiyo inaogoza katika uzalishaji chakula nchini.
“Niwapongeze Shule yenu ya Mnyigumba kwa kujiongeza nakupongeza sana Mkuu kwa kubuni kwa kulima mahindi na kuyatumia kupata chakula kwaajili ua wananfunzi ili wazingatie katika masomo yao” alisema Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile amewataka wanafunzi wa Shule ya Msingi Mnyigumba kuzingatia masomo kwa kusoma kwa bidii kwani wazazi na shule wameamua kuwapatia watoto chakula ili kuongeza ufaulu kwani suala la lishe linasaidia katika kuongeza ufaulu katika shule zetu.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Mnyigumba Bw. Richius Mwamanga amesema kuwa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kimewasaidia katika kuhamisha jamii katika ujenzi wa jiko la shule kwa ajili ya kupikia chakula ambapo limefikia katika hatua ya kupaua.
Ameongeza kuwa Shule imelima shamba la mahindi lililozalisha jumla ya kilo zilizosaidia kutoa chakula kwa wnaanfunzi wa shule hiyo hivyo kusaidia wanafunzi hao kuzingatia masomo na kuongeza ufaulu wao.
“Tunakipongeza na kukishukuru Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba kwa kutoa hamasa na elimu kawa wananchi ili kuhakikisha wanabadili mawazo na kushiriki katika shughuli za maendeleo yao” alisema Bw. Mwamanga.