Kamati ya fedha na uongozi wakiwa katika shule ya msingi Tambukareli .
Baadhi ya madarasa ya Shule ya msingi Tambukareli yanayoendelea kujengwa.
Muonekano wa majengo ya madarasa shule ya msingi Shadi iliyoko Kata ya Luchelele Jijini Mwanza.
Baadhi ya madarasa ya shule ya msingi Kanyerere yaliyokamilika.
…………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza.
Kamati ya Fedha na Uongozi Halmashauri ya Jiji la Mwanza imefanya ziara ya kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo ambapo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo huku ikisisitiza uadilifu katika matumizi ya fedha za serikali.
Kamati hiyo ikiongozwa na Naibu Mstahiki Meya, Bhiku Kotecha imefanya ziara hiyo Leo Jumatatu Novemba 4, 2024 na kukagua miradi mitatu ikiwemo Zahanati ya Mhandu,Shule ya msingi Kanyerere na Shule ya msingi Shadi iliyopo Kata ya Luchelele.
Kotecha alisema miradi hiyo itakapokamilika wananchi watapata huduma bora za elimu na afya.
“Miradi hii inaendelea vizuri na wanaosimamia miradi hiyo wahakikishe wanasimamia vizuri ili thamani ya fedha iweze kuonekana pia tumesisitiza ikamililike kwa wakati ili wananchi wa maeneo haya waweze kupata huduma za elimu na afya karibu”, Alisema Kotecha
Mjumbe wa Kamati hiyo,Charles Nyamasiriri alisema miradi waliyoitembelea hakuna yenye changamoto hivyo ameiomba Halmashauri kuendelea kupeleka fedha kwa wakati ili miradi iweze kukamilika kwa wakati.
Kwaupande wake Mwalimu Mkuu shule ya msingi Tambukareli, Mniko Emmanuel alisema shule ya msingi Kanyerere itakapokamilika itasaidia kupunguza mrundikano wa watoto katika shule yake ambayo inawanafunzi 3245.
“Shule hii itakapokamilika itakuwa na madarasa 13 hadi sasa yaliyokamilika ni matano na itapunguza msongamano katika shule ya msingi tambukareli kwani itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 1500”,