Na Mwandishi wetu
Banki ya Dunia yatoa Semina elekezi kwa Wataalamu wa Mawasiliano kutoka nchi 5 barani Afrika zinazotekeleza Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu (EHPMP) juu ya namna bora ya kufanikisha Mawasiliano katika Mradi hasa katika eneo la utoaji wa elimu juu ya athari zitokanazo na matumizi yasiyo salama ya zebaki (Mercury).
Semina hiyo inafanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 2 hadi 3, 2024 na kuhusisha Wataalamu kutoka nchi za Ghana, Senegal, Zambia, Kenya na mwenyeji Tanzania.
Aidha, Semina hiyo ni utangulizi wa mkutano wa Afika wa nchi wanachama wanaotekeleza mradi huo ambao pia unahusisha masuala ya Usimamizi wa taka za kielektroniki utakaoanza Jumatatu ya Tarehe 4 hadi 12,2024 utakaohusisha nchi hizo 5 pamoja na wadau mbalimbali wa madini na taka za kielektroniki Afrika.