Barabara ya KCMC yafunguka
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Kilimanjaro imekamikisha ujenzi wa barabara ya Kisinane C yenye urefu wa Km. 0.80 kwa kiwango cha lami.
Ujenzi huo ni ahadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Oktoba 2021 alipokuwa kwenye ziara mkoani humo ambapo katika maadhimisho ya miaka 50 ya KCMC, aliyekuwa Mkuu wa Kanisa la KKKT na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Dkt. Fredric Shoo alitoa ombi hilo.
Wakizungumza kwa wakati tofauti baadhi wa wananchuo na wananchi wamesema wamefurahi kukamilika kwa barabara hiyo ambayo ni pana na itawarahisishia kufikisha wagonjwa kwa haraka.
Pia wamesema kufungwa kwa taa hizo zimewaondolea adha ya usalama kwa wanachuo wa KCMC wakati wa usiku wanaporejea mabwenini.
Barabara hiyo ambayo inaingia KCMC ilikamilika mwaka 2023 na mwaka huu wa fedha 2023/2024 TARURA imekamilisha ufungaji wa taa za barabarani ishirini na sita, ujenzi wa mifereji ya maji pamoja na Box Kalavati kubwa moja.