Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Shaaban Ali Othman akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Wizara anayoingoza kutimia Miaka Minne ya Uongozi wa Rais Dk Hussein Ali Mwinyi hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Shaaban Ali Othman akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mafanikio ya Wizara anayoiongoza kutimia Miaka Minne ya Uongozi wa Rais Dk Hussein Ali Mwinyi hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Shaaban Ali Othman akijibu Maswali ya Waandishi wa Habari wakati akizungumzia Mafanikio ya Wizara anayoiongoza kutimia Miaka Minne ya Uongozi wa Rais Dk Hussein Ali Mwinyi hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar.
Muandishi wa Habari wa ZBC TV Ali Rashid Pizaro akiuliza maswali katika Mkutano na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Shaaban Ali Othman akizungumza kuhusiana na Mafanikio ya Wizara anayoiongoza kutimia Miaka Minne ya Uongozi wa Rais Dk Hussein Ali Mwinyi hafla iliofanyika katika Ukumbi wa ZBC TV Mnazi mmoja Zanzibar. (PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.31/10/2024)
……………
Na Khadija Khamis – Maelezo 31/10/2024.
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe. Shaabani Ali Othman amesema jumla ya wananchi 3,577 wamelipwa fidia kutokana na kuathirika na mtetemeko wa ujenzi wa zoezi la uchimbaji mafuta na gesi asilia.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko ukumbi wa Shirika la utangazaji (ZBC) Mnazimmoja wakati akieleza mafanikio ya sekta hiyo ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra ya kutimiza miaka minne ya uongozi wa Dkt. Mwinyi, amesema kati ya wananchi 4,330 sawa na asilimia 83 wameshapatiwa fidia zao.
Amesema mamlaka ya uthibiti na ufuatiliaji mafuta na gesi asilia inaendelea na hatua za ukamilishaji wa asilimia 17 ya wananchi iliyobaki katika ulipaji wa fidia hivyo kwa mwaka wa fedha 2024 hadi 2025.
Aidha amesema wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi imefanikiwa kukamilisha mafanikio mengi ikiwemo soko na diko la kisasa katika eneo la malindi ambalo kwa sasa linahudumia Zaidi ya watu 10,000 kwa siku na boti 350 za uvuvi.
Hatahivyo amesema wizara imefanikiwa kujenga kiwanda cha kusarifu mwani katika eneo la chamanangwe pemba chenye uwezo wa kuchakata tani 30.00 za Mwani mkavu kwa mwaka.
Amefahamisha kuwa katika kipindi cha miaka minne Wizara imefanikiwa kujenga Ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza chakula cha samaki katika eneo la kama chenye uwezo wa kuzalisha tani tano za chakula cha samaki kwa siku pamoja na kukarabati soko la Nungwi Unguja na Tumbe Pemba.
Waziri Shaabani ameeleza kuwa miongoni mwa mafanikio ya miaka minne ni pamoja na Marekebisho ya sheria ya mafuta na gesi asilia ili kuvutia wawekezaji zanzibar
Amesema wizara imefanikiwa kugawa boti 1,927 kwa unguja na pemba kati ya hizo asilimia 70 za vijana na asilimia 90 ya boti za ukulima wa mwani ambazo wanufaika ni mwanawake.
Ameeleza kuwa mapato yatokanayo na tozo katika sekta ya uvuvi na uhifadhi yameengezeka kwa asilimia 262,5 kutoka shilingi bilioni 1.65 katika mwaka 2021 hadi kufikia shilling bilioni 6.0 kwa mwaka 2023
Waziri huyo alitoa wito kwa jamii kuwataka kutoa mashirikiano katika wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi ili iwapo baadhi ya vijiji havijafikiwa na fursa hizo ziweze kufikiwe.