Na Prisca Libaga Arusha
WANARIADHA 500 Kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, Ulaya na Asia watashiriki mbio za Nyuki marathoni zenye urefu wa kilometa 10 na kilometa 21 zitakazofanyika Oktoba 26 kwenye Viwanja vya General Tyre Jijini Arusha.
Rais waTaasisi ya Nyuki Afrika,David Mukomana kutoka Zimbambwe, ameyasema hayo Oktoba 24 kwenye Ukumbi wa mikutano ya kimataifa, AICC alipokuwa akizungumza na Wanahabari kuelezea hatua oliyofikiwa ya maandalizi ya mbio hizo.
Amesema kuwa tayari wanariadha kutoka, Kenya, Uingereza,Uganda,Zimbabwe, Saudi Arabia na wenyeji Tanzania ambao watashiriki mbio hizo zinaojulikana kama ,Apimondia regional Commission for Africa Pesdent yanafanyika kwa mara ya kwanza hapa Nchini.
Amesema lengo la mbio hizo ni kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kutunza nyuki,kuwahifadhi na kuwalinda sanjari na utunzaji mazingira ili kuwezesha nyuki kuendelea kuishi na kuzaliana na ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano mkubwa wa masuala ya Nyuki Ulimwenguni utakaofanyika Nchini mwaka 2027
Taasisi hiyo imetengeneza Programu ya kushirikisha na kuelimisha jamii kuhifadhi na kuwatunza nyukin ili wazalishe asali nyingi kulingana na ongezeko la mahitaji naTanzania ni nchi ya pili barani Afrika kwa uzalishaji wa asali ikitanguliwa na Ethiopia.
Amesema mwakani 2026 mjini Copenhagen nchini Denmark, kutafanyika mkutano wa kimataifa kuhusu masuala ya Nyuki ,ambao una ajenda ya kutoa mwelekeo kwa bara la Afrika na kutaka vijana kushiriki kwenye ufugaji wa nyuki ili wapate vipato.
Amesema nyuki ni viumbe rafiki wana faida nyingi ikiwemo kuzalisha asali,kutoa nta,kutoa dawa za kutibu binadamu pamoja na mapambo mazingira ,hivyo watu wasiuwe nyuki.
Mtendaji Mkuu wa wa taasisi ya Woker Bees Africa, ( WBA) Restetuta Lopes Lazarus, amesema mbio hizo ni kuelezea umuhimu wa nyuki kwa maisha ya binadamu kutokana na umuhimu wake wanatupatia chakula ,asali ambayo ni tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kuboresha kumbukumbu na hiyo ni fursa kwa Wananchi kutunza na kuhifadhi mazingira .
Ally Saburi, ambae ni Mwenyekiti wa Woker Bees Africa,amesema Shirika hilo linajihusisha na ufugaji wa nyuki ikiwa ni kutekeleza malengo 17 ya Umoja wa mataifa hivyo wametengeneza Programu hiyo ya nyuki ambayo ni moja wapo ya malengo hayo ya UN, ambapo nyuki ni zaidi ya asali .
Zipo fursa nyingi zinazotokana na nyuki hivyo kupitia mbio hizo jamii inafikiwa Nyuki imeanzishwa hapa nyumbani mbio hizo ni harakati za kupanua wigo wa ufugaji nyuki,hivyo watatumia mkutano huo wa Denmark kutangaza ufugaji wa nyuki na kuhamasisha mkutano wa 2027 ufanyike Nchini ufugaji wa nyuki una fursa nyingi sana.