Wananchi wa kata ya Chamaguha katika Jimbo la Shinyanga Mjini wamemuomba Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Stephen Julius Masele kusaidia wananchi kutatua changamoto ya kupanda kwa gharama za chakula wakidai wananchi wamekuwa wakishinda na njaa.
Ombi hilo limewasilishwa na Diwani wa Kata ya Chamaguha Mourice Mugini leo Jumamosi Januari 4,2020 wakati mbunge Masele akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa ngazi ya matawi kwenye kata hiyo ikiwa ni mwendezo wa ziara yake aliyoanza Desemba 27,2019 kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Diwani huyo alisema wananchi wake wamekuwa wakishinda na njaa kutokana na wafanyabiashara kupandisha bei ya chakula.
“Mhe. Mbunge changamoto inayotukabili Chamaguha ni njaa. Bei ya chakula imepanda mfano kilo moja ya mahindi inauzwa shilingi 1,100 /=, kilo ya unga wa ugali inauzwa kuanzia shilingi 1,300 hadi 1,500. Tunaomba utusaidie ili bei ya chakula ishuke”,alisema Mugini.
Kufuatia ombi hilo, Masele ameahidi kuzungumza na serikali na mamlaka zingine zinazohusika ili kutumia utaratibu wa siku nyingi ambao umekuwa ukitumika kuwawezewezesha wafanyabiashara wa nafaka kupata mahindi kwa bei nafuu ili wananchi waweze kumudu kununua mahindi kwa gharama nafuu.
Mhe. Masele leo amefanya ziara katika kata ya Kitangili, Ibinzamata na Chamaguha ambapo mbali na kuwapongeza wenyeviti wa serikali za mitaa kuchaguliwa kuongoza wananchi katika uchaguzi uliofanyika Novemba 24,2019, Masele ameendelea kuwasitiza wananchi kupima maeneo yao na kupewa hati ya umiliki wa ardhi ili kuongeza thamani ya ardhi yao.
Mbunge huyo amewataka WanaCCM kushirikiana na kushikamana huku akibainisha kuwa ataendelea kushirikiana na wananchi na serikali katika kuleta maendeleo katika Mji wa Shinyanga ambao sasa unakua kwa kasi baada ya huduma muhimu ikiwemo maji,umeme na barabara za lami kuendelea kusambazwa.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) akimpongeza Diwani wa Kata ya Chamaguha Mhe. Mourice Mugini kwa kutekeleza majukumu yake vizuri katika kata ya Chamaguha leo Jumamosi Januari 4,2020 alipofanya ziara kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuzungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Diwani wa Kata ya Chamaguha Mhe. Mourice Mugini akimweleza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) kuhusu changamoto ya njaa kwenye kata ya Chamaguha kutokana na bei ya vyakula kupanda.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) akizungumza katika kata ya Chamaguha na kuahidi kulitafutia ufumbuzi tatizo la kupanda kwa gharama za chakula.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Chamaguha.
Awali Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Chamaguha Dorica Mong’ateko soma taarifa ya CCM kata ya Chamaguha.
Afisa Mtendaji kata ya Chamaguha,Irene Mshandete akisoma taarifa ya kata ya Chamaguha.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Raphael Patrick Nyambi akizungumza kwenye kikao cha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Chamaguha.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Kitangili.
Wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Kitangili wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM).
Wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Kitangili wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM).
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Kitangili.
Kulia ni Diwani wa Viti Maalumu wilaya ya Shinyanga Mariamu Nyangaka akiwasilisha kero za wananchi wa kata ya Kitangili kwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Kitangili.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ibinzamata.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ibinzamata.
Diwani wa kata ya Ibinzamata akiwasilisha kero za wananchi kwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ibinzamata.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Shinyanga Mjini, Amri Migeyo akizungumza kwenye kikao cha Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Julius Masele (CCM) na wajumbe wa kamati ya siasa CCM ngazi ya matawi na kata ya Ibinzamata.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog