Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Tabora Oktoba 9, 2024 mkoani Tabora.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi, Mohamed Besta akifafanua mchoro wa mradi wa upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Tabora, Oktoba 9, 2024 mkoani Tabora wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile akizungumza na wananchi wa mkoa wa Tabora katika uwanja wa Chipukizi wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango mkoani humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akizungumza na wananchi wa mkoa wa Tabora katika uwanja wa Chipukizi wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango mkoani humo.
Baadhi ya Viongozi mkoani Tabora wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango katika ziara yake mkoani Tabora.