Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Amiri Mkalipa  akizungumza katika mahafali hayo katika.shule ya  mchepuo wa kiingireza  ya Trust .St Patrick iliyopo mkoani Arusha.
Mtawala shule za Trust St.Patrick Schools, Bernadinnah Patrick  akizugumza katika mahafali hayo.
Na.Happy Lazaro,Arusha .

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Amiri Mkalipa amewataka wanafunzi kutumia mitandao ya kijamii  vizuri kwa lengo la kujifunza badala ya kuitumia vibaya jambo ambalo linaharibu  maisha yao. 

Ameyasema hayo  mkoani Arusha wakati  akizungumza katika mahafali ya 16 ya kidato cha nne na mahafali ya 22 darasa  la saba  pamoja  na darasa la awali  katika shule za Trust .St Patrick iliyopo mkoani Arusha .
Amesema kuwa,kumekuwepo na tabia ya wazazi kuwapa watoto simu bila kufuatilia wanachokifanya kwenye mitandao hiyo jambo ambalo mwisho wa siku huwaaribu  watoto hao kutokana na kujifunza vitu  ambavyo  havifai  na kuwaharibia  maisha ,hivyo  kuwataka wazazi hao  kuzungumza na watoto kuhusu matumizi sahihi ya mitandao. 
“wazazi hakikisheni  mnafuatilia kwa karibu matumizi ya simu yanayofanywa  na watoto  wenu kwani wengi wao hutumia mitandao hiyo tofauti jambo ambalo linachangia  kuendelea  kuwepo kwa mporomoko wa maadili. 
Hata hivyo amewataka wazazi hao kuhakikisha wanawafundisha watoto wao kuhusu tamaduni  mbalimbali ili watoto waendelee  kuzienzi  wakiwa tangu wadogo  .
Kwa upande wake  Mtawala shule za Trust St.Patrick Schools, Bernadinnah Patrick  amewataka wazazi kuwa wawazi kuzungumza na  watoto wao kuhusu kuwaambia  hali  halisi ya maisha ilivyo  hivi sasa na kamwe wasione aibu kukemea matukio.mbalimbali kwa watoto hao .
“Hapa shuleni kweli tumekuwa tukitengeneza watoto kuweza kujiajiri wakiwa tangu darasa la nne kwa kuwafundisha bunifu mbalimbali ikiwemo upishi,kilimo, kutengeneza sabuni,keki,na mikate na hata biashara zingine ambapo kupitia programu hiyo tayari wanafunzi 40 walienda nchini China kwa ajili ya kujifunza zaidi kwa vitendo kwa wenzetu.”amesema.
Naye Mmoja wa Wakurugenzi shule za Trust .St.Patrick Schools,Mike Patrick Khanya  amesema kuwa,tangu kuanzishwa kwa shule hiyo ina miaka 27 sasa na imekuwa ikifanya vizuri  kwa wanafunzi katika masomo yote  ikiwemo kuinua vipaji  vya watoto hao kwa kuwapeleka  nje ya nchi kujifunza zaidi kwa vitendo. 
Amesema kuwa,shule  hiyo ina kituo cha michezo ambapo wamekuwa wakiwasaidia wanafunzi kuweza kufanya vizuri kwenye michezo yao  na kuweza kukuza vipaji  kwani michezo  ni ajira. 
Mike amesema kuwa,wamekuwa wakikaa mara kwa mara na watoto wao na kuweza kuwafundisha kuhusu swala zima la mporomoko  wa maadili na kuweza kuwafundisha umuhimu wa kujiheshimu  na kuzingatia nidhamu .