Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma (Katikati) akiwa na watendaji waandamizi wa benki hiyo kwenye picha ya pamoja katika kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma (Katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa sherehe ya wiki ya huduma kwa wateja pamoja naye ni watendaji waandamizi wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma (kushoto) akikata keki pamoja na mmoja ya wateja wa benki hiyo, Bw Conrad leo (Katikati) kwenye sherehe ya wiki ya huduma kwa wateja , kulia ni Wasia Mushi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uendeshaji ) wa benki hiyoMkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma (Katikati) akiwa pamoja na watendaji waandamizi wa benki hiyo kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma wa pili kushoto akitoa zawadi kwa mmoja ya wateja wa benki hiyo , Bw Conrad leo , mwanzo kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uendeshaji ) , Bw Wasia Mushi na mwanzo kushoto ni Mkuu wa Huduma kwa Wateja , Bi Annaroberta Mango
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi, Esther Cecil Maruma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar es Salaam.
………………..
Bank of Africa Tanzania, imeungana na sehemu nyingine duniani katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024, chini ya kauli mbiu “Above and Beyond” na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora wake.
Akizungumza kwenye uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji, Esther Cecil Maruma alisema, “Kwetu Bank of Africa Tanzania, wateja wetu tunawapa kipaumbele kikubwa katika kila mipango tunayofanya. Tunaamini kuwa huduma bora ni zaidi ya kuwapatia huduma za kifedha bali ni kujenga uhusiano mzuri na wa muda mrefu. Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024 ni fursa ya kutambua na kusherehekea imani ya wateja wetu kwetu pia tukithamini kujitoa kwa wafanyakazi wetu wanaofanya kazi bila kuchoka kutoa huduma bora. Tunatarajia kuendelea kutoa huduma zenye viwango vya juu na wigo mpana kuhakikisha tunafikia malengo makubwa”.
Alisema Kauli mbiu ya mwaka huu ya “Above and Beyond” inadhihirisha dhamira ya benki kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja na kukidhi matarajio yao na kuweka msisitizo kwa wafanyakazi wetu kutoa huduma kwa ufanisi mkubwa wa kipekee.
Katika kudhihirisha dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwa karibu zaidi na wateja wake alisema, Bank of Africa Tanzania karibuni ilianzisha huduma ya “BOA Wakala” inayowezesha wateja kuweka na kutoa fedha bila kulazimika kutembelea matawi yake na kuboresha zaidi huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi (B-Mobile) ili iweze kutumiwa na wateja kwa urahisi na kwendana na matakwa yao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa Bank of Africa, Annaroberta Mango, alisema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wafanyakazi wa Benki watapata fursa ya kuongea na wateja kwenye matawi, kupokea maoni yao sambamba na kuwapatia ushauri wa kifedha katika kuimarisha biashara zao.
“Tunajivunia timu yetu ya Wafanyakazi wetu yenye moyo wa kujitolea kufanikisha kutoa huduma bora kwa wateja wetu kila siku. Wiki ya Huduma kwa Wateja pia ni nafasi yetu ya kutambua mchango wao mkubwa. Ni matarajio yetu tutaisherekea pamoja na wateja wetu na kuwashukuru kwa kuichagua Bank of Africa na kuwadhihirishia jinsi tunavyowathamini kwa kuendelea kutuamini,” Mango.
Bw. Conrad Leo, mmoja wa wateja wa Bank of Africa Tanzania customers, alisema amekuwa mteja wa Benki hiyo kwa kipindi cha miaka mitano na anafurahia na kuridhika na huduma zinazotolewa na benki na anapokuwa na changamoto za kibiashara amekuwa akipatiwa suluhisho.
Katika wiki ya Huduma kwa Wateja Benki itakuwa na shughuli mbalimbali zitakazoshirikisha wafanyakazi na wateja ikiwemo kuwashukuru wateja, kuwazawadia wafanyakazi,mafunzo zaidi kwa wafanyakazi kutoa huduma kwa wateja na kushiriki huduma za kijamii na kutoa msaada kwa jamii.