Na Emmanuel Mbatilo
Madereva wa Malori ya Mafuta (Trucker) wameishukuru taasisi ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) kwa kuwafungulia kituo cha kupima mafuta kilichopo Misugusugu mkoani Pwani kwakuwa kimewasaidia kupunguza kero ya kusubiri kupima kwa muda mrefu.
Wamesema uanzishwaji wa kituo hicho umeleta tija kwa sababu kimepunguza sana msongamano wa maroli wakati wa kupima mafuta
Awali tulikuwa tukipima katika kituo cha Ilala ambacho eneo lake ni finyu sana hivyo ilikuwa vigumu sana kumima kwa haraka jambo ambalo lilikuwa likileta kero kwa wasafirishaji wa mafuta.
Kituo hicho kinapima zaidi ya Magali 60 kwa siku kuliko hapo mwanzo katika kituo kilichopo Ilala.
Wamezungumza hayo wakiwa katika harakati za upimaji wa magali yao Misugusugu.