Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi akiwahahihishia na wafanyabiashara wa Sanaa ya ufundi na wachongaji wa vinyago wanaofanya shughuli zao katika kijiji cha mwenge vinyago leo jijini Dar es Salaam kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro wa eneo hilo ndani ya mwaka 2020 alipotembelea eneo hilo kwa ajili kuwataka kuacha kutofautiana kwani hilo ndiyo linalokwamisha kumalizika kwa mgogoro huo.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (wa kwanza kushoto) akitembelea mabanda ya wafanyabiashara wa sanaa za ufundi wanaoendesha shughuli zao katika kijiji cha mwenge vinyago katika ziara yake ya kikazi katika eneo hilo,(wa kwanza kulia) Katibu Mkuu wa Chama cha wachonga vinyago Tanzania Bw.Mintanga Ramadhani.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo akiwahakikishia ushirikiano kutoka wizarani wachongaji wa vinyago na wafanyabiashara wa sanaa ya ufundi wanaoendesha shughuli zako katika eneo la kijiji cha mwenge vinyago alipowatembele jana katika eneo hilo jijini Dar es Salaam,(wa kwanza kulia) Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi.
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania Bw.Adrian Nyangamale akiomba viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kutoa tamko la kulitaka Baraza la Sanaa la Taifa kutoa mwongozo wa kusimamima uendeshaji wa shughuli mbalimbali katika eneo Kijiji cha Mwenge vinyago Jijini Dare s Salaam,walipotembelewa na viongozi wa Wizara hiyo,(wapili kulia) Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi.
Baadhi ya wasanii wa kuchonga vinyago na wafanyabiashara wa sanaa ya ufundi wanaoendesha shughuli zao katika eneo mwenge vinyago wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi (aliyeketi wanne kutoka kulia)mara baada ya kikao na wadau hao katika eneo hilo,(watatu kushoto) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi.Joyce Fisoo na (wakwanza kulia aliyeketi) Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania Bw.Adrian Nyangamale.
……………..
Anitha Jonas – WHUSM,Dar es Salaam
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi amewahikikishia wasanii wanaoendesha shughuli zao katika eneo la Mwenge Vinyago kuwa serikali itahakikisha inamaliza mgogoro wa eneo hilo ndani ya mwaka 2020.
Dkt.Possi ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea eneo hilo la wachogaji wa vinyago na wauzaji wa kazi za sanaa za ufundi lilopo Mtaa wa Nzasa kata ya mwenge kwa lengo la kufahamu ukubwa wa eneo hilo pamoja na kuzungumza na wadau wanaoendesha shughuli zao eneo hilo na kufahamu changamoto zao.
“Eneo hili ni kubwa na nieneo la kimkakati kabisa kuendesha biashara zenu hivyo serikali imedhamiria inatatua kero yenu ya kuwepo kwa mgogoro wa ardhi hii uliyodumu kwa miaka mingi kwani ili kila mmoja wenu aweze kuendesha shughuli zake za kujipatia kipato na hata atakapopatikana mwekezaji basi aweze kuwa huru kuwekeza na kuboresha miundombinu ,“alisema Dkt.Possi.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho na wadau hao Kaimu Katibu Mkuu huyo aliwasahii wadao hao kuacha kuwa na makundi na kutofautiana kwani migogoro hiyo ndiyo itakayokwamisha kukamilika kwa kutatuliwakwa kero za eno hilo hivyo wawe wamoja na waache kumfuatisha huyo anayewajengea chuki miongoni mwao na kuleta mgawanyiko.
Aidha, nae Katibu wa Chama cha Wachogaji wa Vinyago Tanzania Bw.Mintanga Ramadhani alitoa ombi la mazingira ya eneo hilo kuboreshwa katika suala la ulinzi,usafi kwani itasadia wasanii wachongaji wanaofanya shughuli zao kuzifanya kwa ufanisi zaidi na kuongeza ubunifu ambao utalitangaza taifa vyema.
“Ukosefu kwa mafunzo stadi za sanaa ya uchongaji wa na uhaba wa vitendea kazi vya kisasa umekuwa ni kero ya inayokwamisha maendeleo ya kazi hii,”alisema Bw.Ramadhani.
Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo wa CHAMUSATA alitoa maombi ya kwa BASATA kutoa tamko juu ya mwongozo wa matumizi ya eneo hilo sababu ndiyo waliyokabidhiwa kusimamia eneo hilo kwa tamko la Mheshimiwa Waziri Dkt.Harrison Mwakyembe tangu mwaka 2018.
Halikadhalika kwa upande wa Mhasibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa Bw.Onesmo Kayanda aliyemuwakilisha Katibu Mtendaji wa Baraza hilo aliahidi kupokea maelekezo yote yaliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu huyo maara baada ya risala ya chama cha wachongaji vinyago Tanzania kusomwa.