Viongozi wa Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo akiwemo Mwenyekiti wa Shirika hilo Bw. Vicent Kasambala, Padre wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam anayehudumia Wafungwa George Sayi pamoja Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Juma Mgumba wakiwa katika picha ya pamoja wakati Shirika hilo walipotembelea wafungwa na mahabusu Septemba 29, 2024, Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapatia mahitaji ya vitu mbalimbali ikiwemo sabuni ya kuogea, mafuta ya kupakaa, mafuta ya kupikia, dawa ya meno, sabuni, mafuta ya kupikia , viatu pamoja na kushiriki Misa Takatifu katika Gereza hilo ambapo Wafungwa na Mahabusu wamewasihi kuendelea kuwaombea kila wakati ili na wao siku Moja waungane na familia zao. (PICHA NA NOEL RUKANUGA)
Mwenyekiti wa Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo Bw. Vicent Kasambala (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Juma Mgumba mahitaji kwa ajili ya wafungwa na mahabusu wa Gereza hilo.
Padre wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam anayehudumia Wafungwa George Sayi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Juma Mgumba mahitaji kwa ajili ya wafungwa na mahabusu wa Gereza hilo.
Baadhi ya wanachama na viongozi wa Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo wakiwa katika picha ya pamoja Padre wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam anayehudumia Wafungwa George Sayi baada ya kushiriki Misa Takatifu Parokia ya Chang’ombe iliyoambatana na kubariki Mahitaji ya vitu mbalimbali kwa ajili ya kuwapelekea wafungwa na mahabusu katika Gereza la Mahabusu Keko, Dar es Salaam.
Padre wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam anayehudumia Wafungwa George Sayi akibariki mahitaji kwa ajili ya kuwapelekea wafungwa na mahabusu katika Misa Takatifu iliyofanyika Parokia ya Chang’ombe, Jimbo Kuu la Dar es Salaam
………….
Wakristu nchini bila kujali nafasi zao wametakiwa kuwa na hofu ya Mungu kwa kujiepusha kutenda matendo maovu, kuwasaidia wahitaji wenye shida mbalimbali pamoja na kujikita katika kuliweka Taifa katika hali ya amani, maelewano na mshikamano.
Wito huo umetolewa na Padre wa Kanisa Katoliki anayehudumia Wafungwa George Sayi wakati akihubiri katika Ibada iliyofanyika katika Parokia ya Chang’ombe ambayo iliambatana na kubariki Mahitaji mbalimbali ya Wafungwa na Mahabusu waliopo katika Gereza la Keko Dar es salaam vilivyotolewa na Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo Jimbo Kuu la Dar es salaam ambalo linafanyakazi ya kuhudumia watu Masikini, Wagonjwa na Wafungwa kwa lengo la kuadhimisha somo wao Septemba 27 Kila mwaka ambapo amesisitiza Wakristo kuwakumbuka Wafungwa
Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Juma Mgumba, amelishukuru Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo kwa kutoa mahitaji katika gereza hilo, huku akitoa wito kwa jamii kujiepusha kufanya matendo maovu ambayo yatavuruga amani ya Taifa pamoja na kuona umuhimu wa kuwatembelea Wafungwa ili waonje Upendo kutoka kwao na hivyo kubadilisha.
Kwa upande wake Katibu wa Shirika la Mtakatifu Vincent wa Paulo, Chikira Laurence Jahari, amesema kuwa lengo la utume wa shirika hilo ni kuwasaidia wahitaji katika maeneo mbalimbali nchini, huku akieleza kuwa mwaka huu wameona ni vizuri kuwatembelea wafungwa kujua hali zao.
Pamoja na msaada huo wanachama washirika hilo wameshiriki Ibada ya Misa Takatifu katika Gereza hilo ambapo Wafungwa na Mahabusu wamewasihi kuendelea kuwaombea Kila wakati ili na wao siku Moja waungane na familia zao.