Mabigwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga Sc inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mbele ya KMC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Ni mchezo wa kwanza kwa Yanga kucheza uwanja wa nyumbani baada ya kucheza mechi mbili ugenini kwa kuanza na Kagera Sugar 0-2 Yanga, Ken Gold 0-1 Yanga hizi zote ilikuwa ugenini na mchezo wa nyumbani baada ya dakika 90 ubao umesoma Yanga 1-0 KMC.
Mtupiaji ni yuleyule ambaye alianza kufunga ugenini msimu wa 2024/25 Maxi Nzengeli dhidi ya Kagera Sugar amefungua pia pazia la utupiaji kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Ni bao la pili kwa Max alipachika bao hilo dakika ya 4 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo ambapo KMC walicheza kwa tahadhari kubwa kuwakabili mabingwa watetezi wa ligi.
Nyota Ladrack Bocca alichaguliwa kuwa mchezaji bora ikiwa ni mara ya pili mfululizo baada ya kuwa mchezaji bora mchezo uliopita dhidi ya Ken Gold uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Yanga inafikisha pointi 9 baada ya kucheza mechi tatu na zote imeshinda huku safu ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao manne na ukuta haujaruhusu kufungwa ndani ya msimu wa 2024/25.