Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linajulisha kuwa leo Septemba 27, 2024 majira ya saa 2.30 Asubuhi Gari lenye namba za usajili T.601 CFS aina Mitsubishi Fuso Lori likitokea Mbalizi kuelekea kwenye mnada katika Kijiji cha Jojo kilichopo Kata ya Ilembo ilipinduka na kusababisha vifo vya watu 11 ambapo wanaume ni nane (8) na wanawake ni watatu (3), majeruhi 20 kati yao wanaume ni kumi (10) na wanawake ni kumi (10).
Chanzo cha ajali ni dereva kushindwa kuchukuwa tahadhari kwenye mteremko na kusababisha Gari kuacha njia na kupinduka.
Majeruhi bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Ilembo. Dereva alikimbia baada ya ajali na Polisi wanaendelea kumsaka.
Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa madereva kuendelea kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuacha tabia ya kupakia abiria kwenye magari ya mizigo.
Imetolewa na:
Wilbert Siwa – ACP
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa,
Mkoa wa Mbeya.