VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mke wa Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu ya msingi ameamua kuchangia matofali 1300 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili likiwemo darasa la awali pamoja na ujenzi wa darasa moja kwa ajili ya mradi katika shule ya msingi Zegereni iliyopo Kata ya Visiga.
Mama Koka ameamua kuchangia matofali hayo akutokana na kubaini kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa madarasa hivyo amebainisha kuwa kujengwa kwa madarasa mapya kutaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki na kuondokana na adha ya kusoma kwa mlundikano.
Mama Koka amebainisha kwamba anatambua umuhimu mkubwa wa elimu hasa katika wanafunzi wa madarasa ya awali pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi ndio maana akaamua kujikita na kusapoti matofali hayo ambayo matofali 800 yatakwenda kutekeleza mradi wa shule ya awali pamoja na matofali 500 ambayo aliyatoa hapo awali yatatekeleza ujenzi wa darasa moja katika shule hiyo ya msingi Zegereni.
“Katika kuboresha sekta ya elimu mimi kama mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini nimechangia matofali 1300 katika shule ya msingi Zegereni ambapo matofali 800 ambayo yatakwenda kujenga darasa moja la awali na yale mengine matofali 500 yatakwenda kusaidia ujenzi wa darasa moja katika shule ya msingi Zegereni likiwemo la awali ambalo nimechangia matofali 800.
Kadhalika Mama Koka amebaissha kwamba pamoja na kuweza kuchangia matofali pia atahakikisha anasaidia kwa hali na mali katika kuboresha elimu katika shule hiyo ikiwa sambamba na kuahidi kuchangia vitabu mbali mbali hasa katika vitabu vya kiingereza pamoja na hisabati ili kuongeza uwezo zaidi wa wanafunzi kujifunza na kufaulu masomo yao.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Visiga Kambi Legeza amempongeza kwa dhati mke wa Mbunge la Jimbo la Kibaha mjini kwa juhudi zake za kuweza kuchochea na kuchangia matofali katika shule hiyo ya Zegereni na kwamba kukamilika kwa miradi hiyo ya ujenzi wa madarasa kutasaidia zaidi wanafunzi kupata fursa zaidi ya kusoma katika mazingira rafiki na kuongeza kiwango cha ufaulu.
Naye Katibu wa kikundi cha wajasiriamali cha Malkia wa nguvu Bhoke Nyamonge amesema kwamba wao wamesapoti kuchangia matofali 1000 kwa ajili ya kusapoti mradi wa ujenzi kwa wanafunzi wa shule ya awali Zegereni lengo ikiwa ni kuendelea kuunga juhudi za serikali katika kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka amesema kwamba lengo kubwa ni kuhakikisha wanatekeleza Ilana ya chama kwa vitendo hivyo walichokifanya kikundi hicho cha Malkia wa nguvu kinafaa kuigwa na kwamba mke wa Mbunge atawasaidia kwa hali na mali kwa kuwa na yeye ni mjasiriamali.