Na.Alex Sonna.
Mabingwa wa kihistoria timu ya Yanga wameanza kuwatafuta watani zao Simba baada ya kusongea hadi nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu mara baada ya kuichapa bao 1-0 Tanzania Prisons mechi iliyomalizika uwanja wa Samora Mjini Iringa.
Kwa ushindi huu unaifanya Yanga kufikisha alama 21 huku ikiwa imecheza mechi 10 na nafasi ya pili inashikwa na Kagera wenye alama 24 wakiwa wamecheza mechi 13 na Simba wanaongoza wakiwa na alama 28 wakiwa wamecheza mechi 11.
Bao pekee la Yanga SC leo limefungwa na kiungo mshambuliaji raia wa Rwanda, Patrick Sibomana dakika ya tano akimalizia mpira wa kurushwa na kiungo Mzanzibari, Abdulaziz ‘Bui’ Makame kutoka upande wa kulia.
Kikosi cha Tanzania Prisons kilikuwa; Jeremiah Kisubi, Michael Ismail, Laurian Mpalile, Vedastus Mwithambi, Nurdin Chona, Adili Buha, Ismail Aziz/Cleophace Mkandala dk59, Ezekia Mwashilindi/Jumanne Elfadhil dk46, Samson Mbangula, Jeremiah Juma na Benjamin Asukile/Salum Kimenya dk76.
Yanga SC; Metacha Mnata, Mustafa Suleiman, Jaffar Mohamed, Lamine Moro, Ally Mtoni, Abdulaziz Makame/Papy Kabamba Tshishmbi dk68, Deus Kaseke/Mohamed Isa Banka dk84, Feisal Salum, David Molinga, Raphael Daudi/Mrisho Ngassa dk46 na Patrick Sibomana.
Ligi hiyo inatarajia kuendelea kesho kwa Mabingwa Watetezi watakuwa wageni wa KMC mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam