Timu ya Mpira wa miguu ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeshinda magoli 4 dhidi ya Timu RAS Tanga iliyopata goli 1 kwenye mechi iliyochezwa leo tarehe 20 Septemba 2024 kwenye mashindano yanayoendelea Mkoani Morogoro.
Wafungaji wa Mechi hiyo ni Erick Tegamaisho ambaye aliibuka na mpira kwa kufunga magoli 3(hat-trick) na goli 1 lilifungwa na Felician Kavishe.