Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akimkabidhi mashine ya kumsaidia mtoto mchanga kupumua (CPAP) Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Mohammed Mang’una katika tukio lililofanyika leo Septemba 19, 2024 katika Bohari Kuu ya Dawa (MSD) iliyopo Kata ya Keko jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Mavere Tukai (kulia) akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa majukumu yao kwa Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati akikagua utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya MSD.
Picha za matukio mbalimbali wakati Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama alipotembela Bohari Kuu ya Dawa (MSD) iliyopo Kata ya Keko jijini Dar es Salaam.
…………………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amezindua ugawaji wa mashine ya kumsaidia mtoto mchanga kupumua (CPAP) katika hospitali zote nchini, huku akiipongeza Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na muongozo wa Shirika la Afya Duniani kwa kuanza kununua vifaa tiba vya kuokoa maisha ya watoto ambao wapo katika hatari ya kifo baada ya kuzaliwa.
Akizungumza leo Septemba 19, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi mashine 130 za kumsaidia mtoto mchanga kupumua (CPAP) kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, , Mhe. Mhagama, amesema kuwa kuwa Rais Dkt. Samia ataendelea kuboresha sekta ya afya katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuokoa maisha ya mama wajawazito pamoja na watoto wakati wa kujifungua.
Amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa ya kuoa maisha ya mama wajawazito wakati wa kujifungua, kwani takwinu zinaonesha kulikuwa na vifo 530, ambapo kwa sasa vifo vimefikia 104 kati ya wakinamama 1,000 wanaojifungua.
“Ukishamsaidia mama suala linalobaki ni kumuokoa mtoto anayezaliwa na sababu kubwa ya vifo vya watoto wachanga kuzaliwa na uzito pungufu (mtoto njiti) hivyo hana uwezo mdogo wa kupumua ” amesema Mhe. Mhagama.
Amesema kuwa watoo wachanga wamekuwa na uwezo mdogo wa kukabiliana na mazingira, huku akieleza kuwa taarifa za kitafiti duniani zinasema ili uweze kumuokoa mtoto lazima uwe na mashine ya kumsaidia kupumua.
Mhe. Mhagama amesema kuwa asilimia 80 ya watoto wanaozaliwa na uzito mdogo kabla ya muda wanakuwa na tatizo la kupumua.
“Leo tunaweka historia ya kuwa na vifaa tiba ambavyo vinakwenda kutoa mchango mkubwa kwenye uhai wa watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda” amesema Mhe. Mhagama.
Amesisitiza umuhimu wa mashine hizo zinapelekwa katika vituo vyote vya afya, hospitali za wilaya ili kuhakikisha kila kituo cha kinakuwa na mashine tano.
Ametoa wito kwa MSD kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ikiwemo ununuzi, utengenezaji, usambazaji pamoja na kuzingatia ubora wa dawa.
Amesema kuwa lengo ni kuhakikisha dawa zinapatika katika vituo vyote vya afya, huku akibainisha kuwa MSD wanapaswa kuwa na mkakati wa uzalishaji wa dawa ili kupunguza gharama za matibu.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Mavere Tukai, amesema kuwa watahakikisha wanatekeleza kwa wakati majukumu yao kwa kuzingatia uwezo wa taasisi ikiwemo kujenga magala pamoja na kutumia nishati mbadala ili kuipunguzia gharama serikali.
Akizungumza kwa niaba ya Waganga Wakuu, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Dkt. Mohammed Mang’una, wameishukuru serikali kwa kuweza kununua vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto wachanga katika hospitali.