Wadau wa AZAKI wakisikiliza  mada mbalimbali kwenye wiki.ya AZAKI iliyofanyika  mkoani  Arusha kwa wiki.moja
…….
Happy Lazaro,Arusha .
Asasi zisizo za kiraia nchini zimetakiwa kuangalia namna ambavyo wataweza kujitegemea katika kuendesha shughuli mbalimbali za kijamii sambamba na kuendelea kujenga uelewa wa kutosha katika kuchochea uboreshaji katika shughuli za kijamii.
Hayo yamesemwa  mkoani Arusha na Mwenyekiti wa bodi ya AZAKI ,Mercy Silla wakati akifunga wiki ya AZAKI iliyokuwa ikiendelea  kwa muda wa wiki moja mkoani Arusha.
Silla amesema kuwa, kukutanisha asasi hizo wiki nzima wameweza kujadili maswali mbalimbali ya kuboresha katika utendaji kazi sambamba na kujifunza zaidi kutoka kwa wenzao wa nje ya nchi.
Amefafanua kuwa,ni wajibu wao kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele ili kuongeza ushiriki wa kutosha katika shughuli mbalimbali za kijamii na kuhakikisha jamii.unanufaika nazo kwa kiwango kikubwa. 
“Ni wakati wetu  kuhakikisha sasa vijana wetu wananufaika na fursa mbalimbali za kibiashara na kuhakikisha tunajenga uelewa wa kutosha kwa jamii na kamwe tusiache kuchochea uboreshaji ili kuboresha bunifu kwenye mchakato wa kijamii.”amesema Silla.
Amefafanua zaidi kuwa, mkutano huo wa wiki.nzima umeweza kuongeza uelewa wa hali.ya juu kwa vijana na kuweza kuzitambua haki zao ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya kuweza kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo nchini.
Mratibu wa mabadiliko ya tabia nchi kutoka  shirika la Action Aid  Happy Itroz amesema kuwa, kuna  haja ya elimu kutolewa  zaidi kuhusu maswala ya kilimo ikolojia kwani bado kilimo.hicho hakijapewa kipaumbele kwa wakulima kwani kuna mafanikio makubwa sana endapo wakulima watakitumia  .
Hata hivyo ameyataka mabenki kuhakikisha yanatoa  mkopo wa riba nafuu kwa wakulima ili  waweze kunufaika na mkopo na kuweza  kuboresha kilimo chao na kuondokana na kilimo cha mazoea na kulima kilimo chenye  tija  na kuweza kuongeza kipato zaidi.