Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua gari la Huduma Tembezi za Afya (Mobile Medical Service) la Hospitali ya Taifa Muhimbili katika hafla iliyofanyika hospitalini hapo tarehe 12
Septemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati alipowasili Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya kuzindua Kituo cha Upandikizaji wa Mimba pamoja na kuwasha Vifaa vya Kusaidia Kusikia kwa Watoto na Kuzindua Gari la Huduma Tembezi za Afya (Mobile Medical Service)
tarehe 12 Septemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi kuhusu Gari la Huduma Tembezi za Afya (Mobile Medical Service) wakati wa uzinduzi wa gari hilo uliyofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe 12 Septemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Kituo cha Upandikizaji wa Mimba cha Dkt. Samia Suluhu Hassan kilichopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika hafla iliyofanyika hospitalini hapo tarehe 12 Septemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo ya namna ya upandikizaji mimba kutoka kwa Daktari Bingwa wa upandikizaji mimba Dkt. Chuor de Garang Alier wakati akikagua miundombinu ya Kituo cha Upandikizaji wa Mimba cha Dkt. Samia Suluhu Hassan kilichopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mara baada ya kuzindua kituo hicho tarehe 12 Septemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na viongozi mbalimbali wakifurahi pamoja na mtoto Doreen Mtama mara baada ya kuwasha Kifaa cha Kusaidia Kusikia kwa mtoto huyo katika hafla iliyofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe 12 Septemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Viongozi, Wahudumu wa Afya na Wadau wa Sekta ya Afya wakati wa hafla ya kuzindua Kituo cha Upandikizaji wa Mimba, kuwasha Vifaa vya Kusaidia Kusikia kwa Watoto na Kuzindua Gari la Huduma Tembezi za Afya (Mobile Medical Service) iliyofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe 12 Septemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na watoto waliowashiwa vifaa vya kusaidia kusikia pamoja na wazazi wao mara baada ya hafla ya kuzindua Kituo cha Upandikizaji wa Mimba, kuwasha Vifaa vya Kusaidia Kusikia kwa Watoto na Kuzindua Gari la Huduma Tembezi za Afya
(Mobile Medical Service) iliyofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe 12 Septemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Juma Mfinanga wakati akikagua Gari la Huduma Tembezi za Afya (Mobile Medical Service) katika uzinduzi wa gari hilo uliyofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe 12 Septemba 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiondoka katika Kituo cha Upandikizaji wa Mimba cha Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya uzinduzi wa kituo hicho katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe 12 Septemba 2024.
………
Na Sophia Kingimali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amezindua huduma tatu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwemo kituo cha upandikizaji mimba, gari la tiba kwa njia ya mkoba pamoja na kuwasha vifaa vya kusaidia kusikia kwa watoto 15 wenye umri chini ya miaka mitano waliozaliwa na tatizo la kutokusikia huku akitoa rai kwa hospital kuhakikisha wanatunza vifaa hivyo.
Uzinduzi huo umefanyika leo Septemba 12,2024 katika hospital ya Taifa Muhimbili Upanga na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na chama cha Mapinduzi.
Dkt. Mpango amesema uzinduzi wa kituo cha upandikizaji mimba ambacho ni cha kwanza kwa hospitali za umma utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekua wakipata changamoto mbalimbali za kupata watoto.
Amesema huduma hiyo ni maendeleo makubwa kwa hospitali lakini pia ni azma ya serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kibobezi hapa nchini na kwa gharama nafuu.
Akizungumzia kuhusu watoto waliwekewea vifaa vya usikuvu ameitaka hosptali kuhakikisha watoto hao wanasaidiwa kuweza kuongea.
Aidha Dkt Mpango ameipongeza Hospitali hiyo kwa kuweza kujenga jengo hilo la upandikizaji Mimba linaloitwa Samia Suluhu IVF kwa kutumia fedha zao za ndani.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema Serikali imejipanga kuendelea kuboresha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi ili kuwafikia wananchi wengi na kuvutia nchi jirani kuendelea kutumia huduma hizo na hivyo kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kivutio cha utalii tiba.
“Tunahamasisha wataalam wetu sasa twende katika eneo la utalii tiba ili tuweze kuuza huduma hizo kwa mataifa ya nje na pia ninawapongeza madaktari na wauguzi wote wanaotoa tiba bobezi kwa kazi nzuri wanayoifanya katika nchi yetu”, amesema Mhagama.
Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya hospitali hiyo, Dkt. Ellen Senkoro amesema, bodi imeendelea kusimamia na kuboresha hali ya utoaji huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, kuimarisha mifumo ya utoaji huduma, kuboresha miundombinu, kusomesha wataalam na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa dawa kufikia asilimia 98 sasa.
“Sisi kama bodi tutaendelea kusimamia na kuhakikisha huduma hizi zinamfikia kila muhitaji lakini pia vifaa hivi vinaendelea kutunzwa”,amesema.
Hata hivyo,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema mpango wa kuanzisha huduma ya upandikizaji mimba katika hospitali hiyo umetokana na takwimu za changamoto ya uzazi kuzidi kuongezeka siku hadi siku ambapo tafiti mbalimbali duniani zinaonesha kuwa katika changamoto hizo kina baba wanachangia kwa zaidi asilimia 35 huku kina mama ikiwa zaidi ya asilimia 65.