Baadhi ya wakazi
Mkurugenzi wa Mam
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira katika mji wa Mbinga(Mbiuwasa)Mhandisi Yonas Ndomba kushoto,akicheza ngoma ya asili na baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mateka baada ya wakazi hao kupata huduma ya maji ya bomba kwa mara ya kwanza.
………….
Na Muhidin Mwandishi Wetu, Mbinga
BAADHI ya wakazi wa mtaa wa Mateka Halamshauri ya Mji Mbinga mkoani Ruvuma,wameishukuru Serikali kupitia Mamlaka ya maji na usafi w mazingira mji wa Mbinga(Mbiuwasa)kukamilisha mradi wa maji uliokufa zaidi ya miaka 21 iliyopita.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema,kukamilika kwa mradi huo wa maji ya bomba ni ukombozi mkubwa kwa kuwa katika kipindi chote cha miaka 21 walikuwa wanatumia maji ya mto Luwaita ambayo hayakuwa safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Mkazi wa mtaa huo Gido Nomba alisema,kabla ya maboresho ya mradi huo yaliyofanywa na Mbiuwasa huduma ya maji safi na salama ilikuwa changamoto kubwa na walilazimika kwenda Mto Luwaita uliopo umbali wa kilometa 2 kila siku kwenda kuchota maji.
“Tuliwahi kupata mradi wa maji wa Danida,lakini ulikufa kwa muda mfupi tu baada ya chanzo chake kukauka kutokana na ukame uliotokea miaka ya nyuma,tunaipongeza sana Serikali yetu kwa kufanya ukarabati na maboresho ya mradi huu na sasa tunapata maji kwenye kijiji chetu”alisema Nombo.
Agnes Kapinga,amefurahishwa na hatua ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Mbiuwasa kutenga fedha ili kukarabati mradi huo uliosaidia kumaliza changamoto iliyokuwepo kwa muda mrefu.
Aidha alisema,mradi huo umesaidia hata kuboresha maisha yao na kuharakisha maendeleo ya kijiji hicho kwa sababu sasa wanapata muda mwingi kujikita kwenye shughuli za kiuchumi zinazowaingizia kipato.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mji wa Mbinga(Mbiuwasa) Mhandisi Yonas Ndomba alisema,Serikali imetenga kiasi cha Sh.milioni 22 ili kukarabati mradi huo unaohudumia wakazi 3,453 wa mtaa wa Mateka.
Ndomba alisema,katika kijiji hicho kulikuwa na mradi wa maji wa zamani ambao umekufa kwa muda mrefu na hivyo wakazi wa kijiji hicho hawakuwa na huduma ya maji ya bomba badala yake walitegemea kupata maji kwenye vyanzo vyao vya asili.
“kutokana na changamoto hiyo mamlaka tuliona kuna sababu ya kupeleka huduma ya maji na tulianza na usanifu wa mtandao mzima wa maji ikiwemo kukarabati tenki lililojengwa na Shirika la misaada na Denimark na kununua mabomba kwa gharama ya Sh.milioni 22”alisema Ndomba.
Ndomba alieleza kuwa,mkakati wa Mbiuwasa ni kuendelea kuongeza mtandao wa maji kwenye vijiji na mitaa mingine ili wananchi waweze kupata huduma ya maji kwenye maeneo yao.