Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Wawekezaji na Viongozi wa Makampuni mbalimbali ya China Academy of Space Corporation (CASC), China Electronics Corporation, Transsion Group, Weihua Group, China Railway Construction Corporation (CRCC) pamoja na Acme Consultant Engineers PTE Limited na CND jijini Beijing, China tarehe 06 Septemba, 2024, Mhe. Rais yupo nchini China kwenye ziara ya kikazi ambapo alishiriki kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla akizungumza akiwa nchini China.
……………….
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla amesema wizara hiyo ipo tayari kushirikiana na kampuni za wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya mawasiliano nchini.
Alisema hayo jana, akiwa jijini Beijing, nchini China mara baada ya kushiriki mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt.Samia Suluhu Hassan na wawekezaji na viongozi wa kampuni mbalimbali zilizopo China ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi nchini humo.
“Rais alikukutana na kampuni kubwa mbili ambazo zimeonesha nia kutaka kuja kuwekeza kwenye maeneo ya teknolojia nchini kwetu Tanzania katika kampuni hizo mbili moja inahusu masuala ya uwekezaji kwenye satellite.
“Na kampuni nyingine inahusu kuwekeza kwenye masuala ya viwanda na teknolojia ya kutengeneza kompyuta na vifaa vingine vya tehama.
“Rais alifanya mazungumzo hayo na kama tunavyojua sisi nchi yetu tuko kwenye maandalizi ya kutaka kurusha setelaiti yetu kama nchi… sisi kama wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia tumepewa wajibu huo wa kusimamia ili kama nchi tuweze kuwa na satellite yetu.
“Tumeweza kuingia makubaliano ya ushirikiano ya kwenye ujenzi kwa kudizaini satalite yetu kama Tanzania kwa hiyo kwenye mazungumzo ya leo Mh.Rais aliwaahidi kama nchi tuna nia hiyo kama Tanzania kuwa na satellite yetu.
“Na uzuri kama Tanzania tumetengeneza programu ambayo programu hiyo tutaizindua mwaka huu na tumeipa jina ‘From the Peak of Mount Kilimanjaro to Space, kama tunavyojua kama nchi yetu tayari tuna mawasiliano kwenye mlima mkubwa wa Afrika na sasa hivi kilichobaki ni kutengeneza satellite kwenda ‘beyond’
Abdulla alisema wizara iko tayari kushirikiana na wawekezaji hao na imeandaa programu itakayojulikana kwa jina la “From the Peak of Mount Kilimanjaro to Space” itakayohusu uundaji na urushaji wa satelaiti itakayoanza mwaka huu.
Wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza upande wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ni kampuni tatu ambazo ni China Academy of Space Corporation (CASC) inayojishughulisha na masuala ya uundaji na urushaji wa satelaiti.
Katika Mkutano huo, Rais Samia alikuwa na mazungumzo na Viongozi wa Kampuni nyingine ambazo ni China Electronics Corporation iliyoonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vifaa vya TEHAMA pamoja na Kampuni ya Transsion Group Katika mkutano huo, Rais Samia pia amekuwa na mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya China Electronics Corporation, Transsion Group, Huwawei Group, China Railway Construction Corporation (CRCC) pamoja na Acme Consultant Engineers PTE Limited na CND zote za China.
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Watanzania wakiwemo wafanyakazi, wanafunzi na wafanyabiashara wanaoishi nchini China (Diaspora) kwenye mkutano uliofanyika Jijini Beijing Septemba 6, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watanzania wakiwemo wafanyakazi, wanafunzi na wafanyabiashara wanaoishi nchini China (Diaspora) kwenye mkutano uliofanyika Jijini Beijing tarehe 06 Septemba, 2024.