Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akikata rasmi utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji na Umeme katika vijiji vitatu vya Mtavira, Mungaa na
Makotea katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida uliogharimu kiasi cha Shilingi milioni 861 kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Programu ya
Maendeleo (UNDP).
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akimtua mama ndoo kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji utakaohudumia vijiji vitatu vya Mtavira, Mungaa na Makotea katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida uliogharimu kiasi cha Shilingi milioni 861 kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Programu ya
Maendeleo (UNDP).
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akikagua chanzo cha maji cha Mradi wa Maji katika vijiji vitatu vya Mtavira, Mungaa na Makotea katika Halmashauri
ya Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida uliogharimu kiasi cha Shilingi milioni 861 kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Programu ya Maendeleo (UNDP).
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akimkabidhi Cheti cha Shukrani, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Programu ya Maendeleo
(UNDP) nchini Tanzania kwa kufadhili Mradi wa Maji na Umeme katika vijiji vitatu vya Mtavira, Mungaa na Makotea katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, mkoani
Singida kwa gharama ya Shilingi milioni 861.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akimsikiliza Mkuregenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Lawrence Kijazi anayetoa maelezo kuhusu Katibu
Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akikata rasmi utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji na Umeme katika vijiji vitatu vya Mtavira, Mungaa na Makotea.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo akiambatana na viongozi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuelekea kwenye Mradi wa Maji na Umeme katika
vijiji vitatu vya Mtavira, Mungaa na Makotea, mkoani Singida.
******************************
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo amewataka Mameneja wa Mamlaka ya Maji na
Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika mikoa yote 26 wabuni programu maalum itakayomaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji katika vituo vya afya ili kuimarisha huduma zinazotolewa katika maeneo hayo.
Prof. Mkumbo ameielekeza RUWASA kuandaa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha 2020/21 ili kufanikisha utekelezaji wa programu hiyo mahsusi inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika kwenye vituo vyote vya afya nchini, itakayopelekea utoaji wa
huduma bora za afya itakayochochea ustawi na maendeleo ya jamii.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji na Umeme katika vijiji vitatu vya Mtavira, Mungaa na Makotea katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida uliogharimu kiasi cha Shilingi milioni 861 kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Programu ya
Maendeleo (UNDP).
Prof. Mkumbo amesema kumekuwa na malalamiko mengi kwa vituo vya afya kukosa huduma ya maji ya uhakika, jambo ambalo linahatarisha afya za wananchi, ustawi na maendeleo ya taifa kwa ujumla, ikingizatiwa kuwa ni moja ya maeneo muhimu yanayotakiwa kuwa na maji ya
kutosha muda wote ili viweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Aidha, ameishukuru sana UNDP kwa kushiriki katika kuleta maendeleo ya Sekta ya Maji nchini na kusaidia kumaliza tatizo la maji katika Wilaya ya Ikungi iliyokuwa na asilimia 41, kiwango cha chini kabisa cha upatikanaji wa majisafi na salama kwa wilaya zote mkoani Dodoma.
Meneja Mradi, Emmanuel Nko amesema hatua ya utekelezaji wa mradi huo utakaohudumia wakazi zaidi ya 9,000 imekuja baada ya UNDP kubaini uhaba na uhitaji mkubwa wa maji katika vijiji vya Mtavira, Mungaa na Mkotea na umeongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji wilayani Ikungi kwa asilimia 4 mpaka kufikia asilimia 45 kwa sasa.
Ujenzi wa mradi huo unaotumia nishati ya jua una jumla ya vituo 18 vya kuchotea maji, ulianza rasmi Juni, 2019 na kukamilika Disemba 13, 2019.