……………………….
Na Sixmund Begashe-Iringa
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili Kamishna Benedict Wakulyamba ametembelea Makumbusho ya Kalenga ambayo kihistoria ndipo palipokuwa na ngome ya Chifu Mkwawa wa kabila la Wahehe, Mkoani Iringa, na kisha kukutana na Chifu wa Wahehe Adam Abdu Sapi Mkwawa, wazee wa kimila wa kabila la Wahehe, viongozi wa serikali ya Mkoa na wadau wa Malikale.
Katika kikao hicho kilicholenga kupata uelewa mpana juu ya Uhifadhi wa urithi wa Malikale ndani ya Mkoa wa Iringa, CP. Wakulyamba alisema kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na wananchi katika uhifadhi endelevu wa urithi adhimu na adimu wa historia nchini.
Aidha, pamoja na mambo mengine, Wizara kupitia Idara ya Mambo ya Kale iliwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Uhifadhi wa Malikale na ushiriki wa wananchi katika kazi hiyo.