Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi, Zena Said akizungumza jambo wakati akifunga Jukwaa la Wahandisi Vijana jijini Dar es Salaam lililobebwa na kauli mbiu isemayo “Ujasiriamali na Uhandisi, kuongeza Kasi kwa Wahandisi Vijana kufikia Ubora”.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde akisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi, Zena Said wakati akifunga Jukwaa la Wahandisi Vijana jijini Dar es Salaam lililobebwa na kauli mbiu isemayo “Ujasiriamali na Uhandisi, kuongeza Kasi kwa Wahandisi Vijana kufikia Ubora”.
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Bernard Kavishe, akisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi, Zena Said akizungumza jambo wakati akifunga Jukwaa la Wahandisi Vijana jijini Dar es Salaam lililobebwa na kauli mbiu isemayo “Ujasiriamali na Uhandisi, kuongeza Kasi kwa Wahandisi Vijana kufikia Ubora”.
Viongozi na wadau mbalimbali wakisikiliza Hotuba ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi, Zena Said wakati akifunga Jukwaa la Wahandisi Vijana jijini Dar es Salaam lililobebwa na kauli mbiu isemayo “Ujasiriamali na Uhandisi, kuongeza Kasi kwa Wahandisi Vijana kufikia Ubora”.
…………………
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Said amewataka wahandisi vijana kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwewo sekta ya kilimo ili waweze kujiingizia kipato na kujikwamua kiuchumi na sio kutegemea taaluma yao.
Akizungumza leo Septemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifunga Kongamano la Vijana la Ujasiriamali na Uhandisi, Mhandisi Said, amesema kuwa kuna fursa nyingi katika sekta ya kilimo endapo vijana watajikita ili kunufaika kiuchumi na kuondokana na umaskini wa kipato.
Mhandisi Said amesema kuwa zipo zana za kilimo ndogo ndogo ambazo zikitumiwa vizuri zinaweza kubadilisha maisha yao na kuleta tija.
“Shughuli za kufanya zipo nyingi, ni jambo la maamuzi, na sio lazima ufanye jambo moja ili uweze kufanikiwa, tunapaswa kuchangamkia fursa zilizopo nchini” amesema Mhandisi Said.
Amesema kuwa serikali imeweka utaratibu rafiki kwa ajili ya kuwasaidia wananchi ambapo kila halmashauri inatenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwasaidia kiuchumi.
Mhandisi Said amesisitiza umuhimu wa vijana kutumia changamoto zilizopo katika jamii kama fursa ya kutatua na kujiingizia kipato.
“Tunaitaji kuchukua hatua kama wahandisi vijana ili kutumia fursa kupitia ubunifu, ujasiriamali kwa kutumia ujuzi mlionao kuleta mabadiliko chanya katika shughuli zenu binafsi na kuchangia shughuli za Kitaifa” amesema Mhandisi Said.