Sheikh wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hasani Kabeke(wa pili kutoka kulia),akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu (hawappopichani),kabla ya kufungua Mskiti wa Al-Ghazal, Mahina.
Sheikh Hasani Kabeke (Wa pili kutoka kulia) akifungua Msikiti wa Al-Ghazal kwa kukata utepe. 
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakiongozwa na Sheikh Hasani Kabeke,kukagua jengo la Msikiti mpya wa Al-Ghazal, katika Kata ya Mahina.
 
Sheikh wa Wilaya ya Nyamagana,Ramadhan Ndaki (kulia), akizungumza kabla ya kufunguliwa kwa Msikiti wa Al-Ghazal Mahina.
Alhaji Hasani Kabeke, leo akisaini kitabu cha wageni kabla ya kufungua Msikiti wa Al-Ghazal Mahina.
 
Akinamama wa dini ya Kiislamu hawakuwa nyuma katika kushuhudia ufunguzi wa Msikiti wa Al-Ghazal, Mahina, 
…………. 

NA BALTAZAR MASHAKA,MWANZA

SHEIKH wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Hasani Kabeke,amefungua Msikiti wa Al-Ghazal  katika Kata ya Mahina,Wilayani Nyamagana na kuwataka waislamu kutosikiliza maneno ya kuwavunja moyo katika kujiletea maendeleo.
Tukio hilo la kihistoria limefanyika leo Agosti 19,2024 kwa kufungua msikiti huo mpya baada ya msikiti wa zamani kuvunjwa ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa ya kiwango cha kimataifa ya treni ya mwendo kasi (SGR)
Akizungumza katika hafla hiyo Sheikh Kabeke amesema waislamu waache kusikiliza maneno ya ovyo yenye kuwatisha tamaa katika kuchangia miradi na kujieletea maendeleo yao.

“Tukio hili ni la kihistoria la kufungua Msikiti huu wa Al-Ghazal Mahina,yalisemwa mengi kuhusu fedha za ujenzi wa msikiti huu lakini leo msikiti umefunguliwa wa kisasa baada ya kuvunjwa wa zamani kupisha mradi wa SGR,”amesema bila kufafanua.

Sheikh Kabeke amewataka wasaidizi wake waendelee na mwendo wa kuziba masikio mithiri ya chura kiziwi ili wawaleletee waislamu maendeleo wana Mwanza kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Sheikh  huyo wa Mkoa wa Mwanza,BAKWATA chini ya Mufti Dk.Sheikh Abubakar Bin Zubeir Bin Ally  Mbwana ( Mujaddidul asri),inafanya kazi kwa uadilifu uliojaa uaminifu ingawa mapungufu kwa mwanadamu hayakosekani,hivyo jitihada zaidi za kukifanya chombo hicho kiendelee kuwatumikia waislaam zinafanyika.

 Aidha Alhaji Kabeke ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita na kummwagia sifa Rais Dk.Samia Suluhu Hassam kwa kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo SGR. 

Katika hatua nyingine Alhaji Kabeke ameongoza dua kumuombea Rais Samia,Mufti na Sheikh Mkuu  wa Tanzania na wote waliosimama imara kusimimia fedha za fidia zilizotolewa na serikali na  kuwezesha kupatikana msikiti mzuri wa Kisasa,Madrasa nzuri ya kisasa na ofisi nzuri, kuw Mwenyezi Mungu awabarikie.sss