Katibu Mkuu ofisi ya Rais Utumishi ,Xavier Daud akizungumza katika mkutano huo mkoani Arusha .

…………………

Happy  Lazaro,Arusha .

Arusha .Katibu Mkuu ofisi ya Rais Utumishi ,Xavier Daud amesisitiza taasisi za nchi wanachama wa (ESARBICA)  kutumia teknolojia zenye mfumo wa kisasa wa  utunzaji wa Nyaraka na kumbukumbu ili kuendana na teknolojia na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi

Ameyasema hayo leo mkoani Arusha katika mkutano  wa 59  wa nchi  wanachama  wa bodi ya baraza la wahifadhi nyaraka kusini mashariki Afrika (ESARBICA) uliozihusisha taasisi zinazohusika na utunzajia wa kumbukumbu na nyaraka.

Aidha amesisitiza kwamba kwa asili utunzaji  wa nyaraka  ulikuwa wa kawaida lakini kwa sasa hivi  hali imebadilika  na kuwa ya sayansi na teknolojia na kusababisha ufanisi kuongezeka kwa maana ya kuwa mnawasiliana haraka.

“Tunasisitiza kwamba baada ya mabadiliko ya teknolojia tutoke kwenye utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za serikali za makaratasi ,kama tunavyojua nyaraka na kumbukumbu ni moyo wa serikali unapotunza nyaraka  zako kidigitali unakuwa na ufanisi zaidi  katika utendaji kazi .”amesema.

Aidha alisisitiza taasisi za nchi wanachama  na nchi ya Tanzania kuendelea kutumia mifumo  hiyo ya kisasa .

Amefafanua kuwa,kutokana na mabadiliko  ya kimfumo  alisisitiza  kuwepo kwa wataalamu   wazawa  na wazalendo ili wenye kuweza kumiliki  mifumo yetu ili kuweza kudhibiti mifumo hiyo .

Naye Mkurugenzi ofisi ya Rais idara ya kumbukumbu na nyaraka za Taifa ,Firimin  Msiangi  amesema kuwa kazi ya bodi  ni kubadilishana uzoefu katika kuhakikisha sekta hiyo inaboreshwa na katika kuhakikisha kumbukumbu  na nyaraka  za serikali katika nchi yetu  inatunzwa vizuri na kutoa huduma bora kwa wananchi .

“Katika eneo hili  kila nchi ina uzoefu wake ndio maana tumekutana hapa kwa ajili ya kubadilishana uzoefu “amesema Msiangi.

Amefafanua kuwa,  katika mkutano huo nchi zilizoshiriki ni 14 kati ya nchi 15 wanachama na wanaendelea kuzihamasisha nchi zingine kushiriki katika mkutano huo  .

Amesema kuwa,pamoja na mambo mengine mkutano huo utajadili namna wanavyoondoka kwenye matumizi  ya nyaraka za karatasi kwenda kidigitali ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma bora  kwa wananchi na serikali kwa ujumla .

Kwa upande wake Rais wa ESARBICA ,Puleng Kekana kutoka nchini Afrika kusini  amesema kuwa ,serikali imeanzisha usimamizi wa kumbukumbu za kidijitali na mfumo wa uhifadhi ambapo mkakati wa kuhifadhi kumbukumbu, 

Amesema kuwa ,wakati wa kutekeleza upatikanaji wa kumbukumbu inapohitajika na watumiaji, kumbukumbu za Taifa daima zimeendelea kushirikiana na baadhi ya taasisi za umma, ikiwa ni pamoja na wizara, mashirika ya serikali, kuweka kumbukumbu zao kwa madhumuni ya kuhifadhi na kupatikana kwa maamuzi kwa wakati .

Kekana amefafanua kuwa,mashirika tuliyonayo yanapaswa kuhakikisha kuwa nchi wanachama zinachukua hatua madhubuti za kuandaa na kutekeleza programu za mafunzo kwa taaluma za kumbukumbu, haswa vijana,  huku akiwataka wanaharakati  kuhakikisha  taasisi za kitaaluma katika kanda zinaboresha mitaala yao ya kumbukumbu na usimamizi wa kumbukumbu ili kuendana na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano katika usimamizi wa kumbukumbu .