Mkurugenzi wa huduma za kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi.
Waganga wakuu wa wilaya,Wafamasia na waratibu wa Malaria kutoka mikoa na wilaya za Iringa,Njombe,Morogoro,Dodoma na Singida wakiwa kwenye kikao kazi hicho kinachofanyika jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha tathimini ya utekelezaji wa shughuli za malaria
Washiriki wa kikao kazi cha kutathimini utekelezaji wa shughuli za malaria wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye kikao hicho ikiwa na lengo la kuondoa ugonjwa wa Malaria nchini.
………………………………………………..
Na. Catherine Sungura, Dodoma
Kiwango cha ugonjwa wa Malaria nchini kimepungua zaidi ya asilimia hamsini ndani ya miaka miwili kutoka asilimia 14 mwaka 2015 hadi asilimia 7.3 kwa mwaka 2017.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa huduma za kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi wakati wa kikao kazi cha kanda kinachojumisha,waganga wakuu wa mikoa,wilaya, wafamasia na waratibu wa malaria kutoka kanda tano za mikoa ya Kikao hico kinajumuisha mikao ya Dodoma, Singida,Njombe,Iringa na Morogoro.
Dkt. subi amesema kuwa mkutano huo wa kanda una lengo la kutathimini utekelezaji wa shughuli za Malaria kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria (NMCP) “tumedhamiria kuitokomeza na kuondoa kabisa Malaria Tanzania na mafanikio yameanza kuonekana kwa kipindi cha miaka kumi sasa kwani mwaka 2010 kiwango cha Malaria kilikuwa asilimia 18 lakini hivi sasa tunaongelea asilimia 7.3”.
Amesema kuwa vifo vitokananvyo na Malaria navyo vimepungua kwa zaidi ya asilimia 75 kwa zaidi ya miaka kumi, vile vile watu wanaougua Malaria na maambukizi mapya nao wamepungua kwa zaidi ya asilimia 67.
“Lakini Tanzania bado tunatajwa kama nchi yenye kiwango kikubwa chenye Malaria katika nchi za Afrika mojawapo kati ya nchi kumi ila bado tunayo fursa ya kuiondosha Malaria hapa nchini”.
Aidha, Dkt. Subi amesema kuwa kama nchi hivi sana wanataka kuwa na mpango endelevu wa kuondoa Malaria ambao utasaidia kuondosha malaria kuanzia viluilui pamoja na mbu wapevu.
“hawa mbu tukipambana kuwaondosha tutaweza kuiondoa Malaria nchini kwani tunayo fursa kwa kutumia kiwanda chetu cha kibaha ambacho kinazalisha viuadudu, hivyo tutaendelea kununua pia kusambaza viadudu kwenye ngazi za halmashauri pamoja na kutumia njia ya jamii kwa kila mtaa na vijiji.
Kwa upande wa binadamu Dkt. Subi amesema mpango huo utataka kila atakayeenda kwenye kituo cha kutoa huduma za afya akipimwa na akigundulika na Malaria na kupata tiba atafuatiliwa “tunataka kila atakayeenda kituo chetu cha huduma apimwe, apate tiba sahii na baada ya tiba afuatiliwe mana watu wengi tukiwapatia dozi hakuna anayejua kama mtu huyo kiwango cha Malaria kimeisha na anaendelea vizuri ili watu katika familia yake wasiambukizwe”Alisisitiza Dkt. Subi.
Hata hivyo ameitaka mikoa kuhakikisha inatenga fedha kwa ajili ya udhibiti wa mvu na wadudu wadhurifu na kuzingatia miongozo ya Wizara katika kudhibiti ugonjwa wa malaria nchini kwani lengo lililoweka ifikapo mwaka 2020 ni kufikia angalau asilimia moja.