********************************
Serikali mkoani Njombe imeongeza muda wa mwezi mmoja na siku mbili kwa wadaiwa sugu wa vyama vya ushirika kurejesha fedha walizokopa katika vyama hivyo vinginevyo watakamatwa na kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi kama wahujumu wengine wa taifa.
Akizungumza na wadaiwa sugu wa vyama hivyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Katarina Revokati ambaye ni katibu tawala mkoani humo anasema hadi kufikia desemba 18 fedha iliyorejeshwa ni mil 6.6 kati ya bil 6.4 ambazo zilikopwa katika vyama 336 miaka kadhaa iliyopita na kueleza kuwa serikali imeongeza muda ili kuepusha visingizio pindi kamata kamata itakapofanyika na vyombo vya ulinzi na usalama.
Katika zoezi la kurejesha fedha hizo mkuu wa mkoa ameunda vikosi kazi vidogo vinavyoongozwa na wakuu wa wilaya ambavyo vinavyokwenda kushirikiana na kikosi kazi cha mkoa na hivi ndiyo mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrew Tsere na Ruth Msafiri wa wilaya ya Njombe wanavyotoa msimamo wao kwamba watahakikisha fedha zote zinarudi na kuanza kunufaisha wananchi .
Nae Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa anasema fedha ya umma haiwezi kuliwa na wajanja wachache hivyo wanakwenda kuifanya kazi ipasavyo ili kunusuru ushirika.