Dodoma
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatius Mtavila amewataka wananchi kuhakikisha wanachagua viongozi bora watakaosaidia kusimamia utunzaji wa miundombinu ya barabara kwenye maeneo yao.
Ameyasema hayo alipotembelea banda la TARURA kwenye Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.
Mhadisi Mtavila amefafanua kuwa Serikali imejenga barabara zenye urefu wa kilometa 144,130 kwenye maeneo ya vijijini hivyo miundombinu hiyo inahitajika kutunzwa na kulindwa na wananchi ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
“Kuna changamoto nyingi kwenye maeneo ya vijijini hasa katika suala zima la utunzaji wa barabara, wananchi wengi wanapitisha mifugo kwenye miundombinu hiyo jambo ambalo linasababisha uharibifu mkubwa wa barabara na hali hii hupelekea barabara nyingi kukatika, hivyo tunahitaji viongozi imara watakaosimamia