Afisa mauzo kutoka kampuni hiyo,Andrew Vitalis wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu bidhaa zao katika maonyesho ya nanenane Njiro
…………….
Happy Lazaro, Arusha .
KAMPUNI ya TROUW NUTRITION kutoka nchini Uholanzi inayohusika na lishe ya Mifugo imejipanga kutoa elimu kwa wafugaji kutoka mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara kuhusu ufugaji bora wa kisasa na wenye tija.
Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Afisa mauzo kutoka kampuni hiyo,Andrew Vitalis wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea mkoani Arusha.
Vitalis amesema kuwa,kampuni hiyo imekuwa mkombozi wa wafugaji kwa kutoa elimu kuhusu ufugaji bora wa kisasa ambapo wana bidhaa bora sana za kisasa ambazo zinasaidia dhidi ya vimelea vya magonjwa.
“Wafugaji wamenufaika wengi sana kupitia kampuni yetu hii kutokana na lishe bora tunazozalisha ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa sana na kuwawezesha wafugaji kuweza kupata mara dufu.”amesema .
Aidh amefafanua zaidi kuwa, kampuni hiyo imekuja na bidhaa bora kabisa ya Selko Alpha ambayo ni mchanganyiko wa Organic Acids ambayo hupunguza pH ya maji ya Mifugo na utu mbo wa mnyama kwa haraka zaidi baada ya kuweza chakula na inaboresha usawa wa microbial katika njia ya utumbo.
Ameongeza kuwa, bidhaa zao zimekidhi viwango vya kimataifa ambapo bidhaa hizo hutumika nje ya nchi kwa kiwango kikubwa kutokana na ubora wake uliopo .
Aidha ametoa wito kwa wafugaji kutembelea banda lao ili kuweza kupata elimu ya kutosha namna ya ufugaji bora na wa kisasa na wenye tija ya kiwango cha juu na kuweza kukutana na wataalamu wabobezi wa viwango vya juu .
“Sisi tunatoa elimu namna ya kutengeneza chakula cha Mifugo kwa gharama nafuu kuweza kupunguza matumizi ya madawa katika ufugaji. “amesema .