Bi. Asumpta Muna Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Chuo cha Benki Mwanza akizungumza na Fullshangwe katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika Nzuguni jijini Dodoma.
…………
Chuo cha Benki Mwanza kimemeendela kuwajenga wanafunzi kwenye maadili ili kuhakikisha wanawapata watendaji wazuri watakaosimamia suala la maadili katika sekta ya fedha.
Hayo yamebainishwa Leo Agosti 3, 2024 na Bi. Asumpta Muna Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Chuo cha Benki Mwanza Wakati akizungumza na Fullshangwe Blog katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea kufanyika Nzuguni Jijini Dodoma.
Amesema chuo hicho kinamajukumu ya kutoa elimu kwa umma kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi sanjari na sula la maadili.
Ameeleza kuwa mafunzo ya muda mfupi ni kuwajengea uwezo wafanyakazi walioko kwenye sekta ya fedha ili waendelee kuongeza weledi na ujuzi utakao leta tija katika kazi zao.
“Kutokana na mafunzo haya kuwa mahili pia yamevutia nchi jirani ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Msumbiji,Ghana, Malawi, Zambia hizi ni baadhi ya nchi ambazo zimekuwa zikileta washiriki kutoka katika benki kuu za nchi hizo kuja kufanya mafunzo katika Chuo chetu kwa lengo la kuendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi wao”, amesema
Amesema Chuo hicho kinatoa mafunzo ya muda mrefu katika kozi mbili ikiwemo astashaada ambayo ni kozi ya miaka miwili na tunachukua wanafunzi ambao wamemaliza kidato cha sita ambao wana malengo ya kufanya kazi katika sekta ya fedha.
Aidha, amesema kuwa Chuo hicho kimefungua dirisha la udahili ambao unaendelea hadi mwezi wa tisa hivyo wanawakaribisha watu wote wanaohitaji kujiunga kwa ajili ya kufanya udahili.