Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi akiongea na watumishi wa Taasisi hiyo wakati wa ziara ya kikazi Julai 30,2024 ikiwa ni ziara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo Mei 15,2024.
Watumishi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wakimsikiliza Mwenyekiti mpya wa Baraza la Uongozi wa Taasisi Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi (hayupo katika picha) wakati wa ziara ya kikazi Julai 30,2024 ikiwa ni ziara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo Mei 15,2024.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi (wa kwanza Kushoto) akiwa katika studio za Nelson Mandela radio kwa masafa ya 98.9 fm ambayo kwa sasa ipo hewani kwa njia ya mtandao (online) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Taasisi hiyo Julai 30,2024, wa pili Kushoto ni Kaimu Makumu Mwenyekiti Bw. Sylvester Kazi, Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula wa tatu Kushoto na Mkuu wa Kituo cha Umahiri cha WISE-FUTURE Prof. Hans Komakech wa kwanza kulia.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi ( wa pili kulia) akipata maelezo kuhusu Kituo Atamizi kutoka kwa Dkt. Josephine Mkunda (wa kwanza kulia) wakati wa ziara ya kikazi Julai 30,2024, wengine ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula (wa pili kulia) na Kaimu Makamu Mwenyekiti Bw. Sylvester Kazi ( wa kwanza Kushoto).
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi ( mwenye miwani) akipata maelezo kuhusu Komputa yenye Uwezo Mkubwa wa kuchakata data (HPC) kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha Tehama Bw. Mdoe Mwamunyange (Kulia) wakati wa ziara ya kikazi Julai 30,2024.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi (wa pili kushoto) akipata maelezo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Mabweni ya Wanafunzi kutoka kwa Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula (Kushoto) wakati wa ziara ya kikazi Julai 30,2024.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kuhusu bidhaa zinazozalishwa katika Kiwanda Kidogo cha DDI kilichopo katika Taasisi hiyo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula(Kulia) wakati wa ziara ya kikazi Julai 30,2024.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Taasisi wakati wa ziara ya kikazi Julai 30,2024.
………………
Na Mwandishi Wetu-Arusha
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi ametoa wito kwa watumishi wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na umakini kwa kuzingatia dira na dhamira ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo ili kwa pamoja kutumia fursa zilizopo katika kutatua changamoto mbalimbali.
Mhe. Balozi Maimuna ameyasema hayo Julai 30, 2024 wakati wa kikao na watumishi wa taasisi hiyo, ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kikazi tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo Mei 15, 2024.
“Taasisi hii ni ya kipekee yenye kuleta umuhimu wa dhana nzima ya kuanzishwa kwake, na ipo fursa ya sisi kufanya zaidi ili ule upekee wake uzidi kuonekana waziwazi” Mhe. Balozi Maimuna
Aidha Mhe.Balozi Maimuna aliahidi kushirikiana na viongozi katika kuhamasisha watoto wa kike kujiunga na masomo ya sayansi katika ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu ili kuwa na idadi kubwa ya wanawake katika nyanja ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na ubunifu.
” Ili mtoto wa kike aweze kusonga mbele ni muhimu kuhakikisha kuwa ameingia kikamilifu katika Sayansi, teknolojia na ubunifu ” amesema Mhe. Balozi Maimuna.
Mhe. Balozi Maimuna Kibenga Tarishi alipokea taarifa fupi ya taasisi kutoka kwa Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula na kupata wasaa wa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Kituo cha Elimu Kidigitali( C-CoDE), Maktaba, Maabara, Kituo cha Tehama (HPC) , Kituo Atamizi, Kiwanda Kidogo (DDI) na Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi.
Naye Mkuu wa Taasisi Bw. Omari Issa akizungumza kwa njia ya mtandao kutoka Washington nchini Marekani alimkaribisha Mwenyekiti huyo na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu ya kuhakikisha dira na dhamira ya taasisi inafikiwa kwa mafanikio makubwa.