Jamii imetakiwa kuienzi siku ya mashujaa kwa kuhakikisha inafanya shughuli mbalimbali zenye manufaa kwa umma
Rai hiyo imetolewa na muwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Katibu tawala Wakili Bi Mariam Abubakar Msengi wakati wa zoezi la kufanya usafi katika kituo cha afya Buswelu kama sehemu ya kumbukizi ya siku ya mashujaa ambapo akawaasa kuitambua na kuithamini siku hiyo muhimu kwa taifa
‘.. Kila julai 25 ya mwaka tunawakumbuka mashujaa wetu waliojitoa maisha yao Kwa taifa letu, Sasa niwaombe wananchi tuienzi hii siku na tuijali ..’ Alisema
Aidha Wakili Bi Msengi amewasisitiza wananchi kujitokeza na kushiriki shughuli za maendeleo sanjari na kumshukuru Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan kwa fedha za miradi ya maendeleo
Kwa upande wake diwani wa kata ya Buswelu Mhe Sara Ng’wani ameshukuru uongozi wa wilaya ya Ilemela kwa kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi ndani ya kata yake huku akiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika maendeleo
Dkt Maria Kapinga ni mganga mkuu wa wilaya ya Ilemela ambapo amesema kuwa pamoja na tendo la kufanya usafi wao kama idara ya afya wataendesha zoezi la upimaji wa magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza bure bila gharama yeyote kama shinikizo la damu, hali ya lishe, ukimwi, kisukari na macho kwa siku mbili mfulilizo ya leo na kesho hivyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi