Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Said Side akizungumza na mamia ya wakazi wa Kata ya Pugu Steshen waliojitokea kwenye Mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa Kata hiyo Shaban Mussa.
Diwani wa Kata ya Pugu Stesheni jijini Dar es salaam Shaban Mussa akizungumza na mamia ya wakazi wa Kata ya Pugu Steshen waliojitokea kwenye Mkutano wa hadhara ambao umefanyika kwenye Kata hiyo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Said Side,akigawa vifaa vya michezo na jezi kwa vijana wa timu mbalimbali za michezo kwenye Mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa Kata ya Pugu Steshen Shaban Mussa.
Diwani wa Kata ya Pugu Stesheni jijini Dar es salaam Shaban Mussa (kushoto) akiwa sambamba na Afisa Mtendaji wa Kata ya Pugu stesheni kwenye Mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa Kata ya Pugu Steshen Shaban Mussa.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Pugu Stesheni na wanachama wa Chama cha Mapinduzi ambao wamehudhiria katika kwenye Mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa Kata ya Pugu Steshen Shaban Mussa.
…………
NA MUSSA KHALID
Wakazi wa Kata ya Pugu Stesheni jijini Dar es salaam wametakiwa kuendelea kumuunga Mkono Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan,Wabunge na wenyeviti wa mitaa katika Kata yao ili waweze kufanya kazi zao Kwa ufanisi na ujasiri ili maendeleo katika maeneo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Said Side wakati aliposhiriki kwenye Mkutano wa hadhara katika Kata hiyo inayoongozwa na Diwani Shaban Mussa na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.
Mwenyekiti huyo amewasisitiza wananchi hao kufahamu kuwa Maendeleo yanayofanyika katika Kata yao yanatokana na uimara wa Viongozi waowaliowachagua.
Aidha amesema kuwa lengo la Chama hicho ni kuhakikisha wanaisimamia vyema serikali Ili yale waliyoohidi kupitia Viongozi mbalimbali yaweze kutekelezeka kwa wakati na muda uliopangwa.
“Si Madiwani wote wanawajibika kama alivyo Mhe Shabani Hivyo Pugu Stephen mumempata Kiongozi mahiri ambaye anapambana kuwaondolea changamoto katika maeneo yenu hivyo musisite kumuonyesha ushirikiano Kila wakati sambamba na Viongozi wengine waliopo katika Kata yenu.”amesema Side
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Pugu Stesheni Shaban Mussa amesema mafanikio yanayoonekana katika Kata hiyo yanatokana na ushirikiano aliojenga na watendaji wote katika kusimamia vyema miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Diwani huyo amesema amefanikisha kuboresha miundombinu ya shule za Sekondari na Mazingira huku akiahiri kwa kushirikia na serikali ataendelea kuhakikisha changamoto zilizopo katika baadhi ya maeneo wanazipatia ufumbuzi.
Katika Hatua nyingine Diwani huyo amewataka wananchi wa Pugu Stephen kuzingatia sera ya ulinzi na Usalama Ili kuepukana na changamoto ya wahalifu katika maeneo yao.
Kwa upande wao,Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Pugu Stephen William Kabonda na Madam Zawadi Kondo,Makamu Mkuu wa Shule wa Bangulo licha ya kupongeza jitihada za Diwani huyo wamesema wanakumbana na changamoto ikiwemo miundombinu mibovu ya madarasa pamoja na upungufu wa walimu,pia Kuna ukosefu wa Maktaba ya shule