Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Dk.Alhaji Sibtain Meghjee (wa pili kutoka kushoto),leo akiwa na maofisa wa Gereza Kuu la Butimba, baada ya kukabidhi miundombinu ya maji katika gereza hilo.
Sheikh wa Bilal Muslim Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hashim Ramadhan (mbele) akiongoza maandamano ya waumini wa madhehebu ya Shia Ithansheria jijini humu, leo wakiadhimisha Siku ya Ashura ikiwa ni kumbukizi ya kifo cha Imamu Hussein Ibn Ali.
Baadhi ya masheikhe wa Bilal Muslim mkoani Mwanza, wakishiriki maandamano ya kukimbukizi ya Kifo cha Imamu Hussein Ibn Ali, leo.
Vijana wa dhehebu la Waislamu wa Shia Ithnasheria wakiwa wameshika bango lenye ujumbe ‘Kukaa kimya mbele ya Ufisadi ni sawa na kukubali dhuluma.’, wakati wa maandamano ya Siku ya Ahura jijini Mwanza.
Akina mama wa Kiislamu wa Shia Ithnasheri wakiandamnana jijini Mwanza leo katika kudhimisha Siku ya Ashura wakikumbuka kifo cha Imamu Hussein Ibn Ali, mjukuu wa Mtume Muhhamad S.A.W. aliyeuawa huko Karbala miongo kadhaa. (Picha zote na Baltazar Mashaka)
……….
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
TAASISI ya The Desk & Chair Foundation katika kuadhimisha siku ya Ashura, leo imefadhili matangi matano ya kuhifadhi maji safi na mabomba ya mita 300 yenye upana wa inchi 2 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya maji safi na salama katika Gereza Kuu la Butimba mkoani Mwanza .
Aidha taasisi hiyo hivi karibuni imechimba na kujenga kisima kirefu katika eneo la Gereza hilo la Butimba kitakachowahudumia watu takribani 3,000 kwa siku wakiwemo wafungwa, watumishi wa gereza na familia zao.
Kupatikana kwa huduma ya maji katika gereza hilo kutawaondolea watumishi, wafungwa na mahabusu changamoto ya uhaba wa maji kwa matumizi mbalimbali.
Taasisi hiyo imewashukuru wafadhili wote kwa kuwezesha miradi hiyo ya kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kiuchumi.
Katika hatua nyingine waumini wa dhehebu la Shia Ithna Sheria jijini Mwanza, wameadhimisha Siku ya Ashura kwa maandamano ikiwa ni kukimbikizi ya kifo cha Imamu Hussein Ibn Ali aliyeuawa katika ardhi ya Karbala.
Imamu Hussein ambaye ni Mjukuu wa Mtume Muhhamad S.A.W.anatajwa kuwa Imamu wa kwanza wa dini ya Kiislamu ya dhehebu la Shia, aliuawa pamoja na wengi wa watu wa familia yake.
Taasisi ya The Desk & Chair Foundation kila mwaka imekuwa ikiadhimisha siku ya kifo cha Imamu Hussein kwa kupanda miti ama kuchimba kisima cha maji kwa ajili ya kusaidia jamii ikiwa ni kumbukumbu ya namna Imamu huyo alivyozingirwa na watesi wake na kunyimwa maji ya kunywa.
Pia waumini wa dhehebu hilo wamekuwa wakimkumbuka Imamu Hussein kwa kufanya mambo mbalimbali ya kijamii kama kupanda miti na kuchimba visima vya maji