Mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa bandari ya Nyamirembe Chato , Injinia Anderson Mbogowe akitoa maelezo kwa Injinia wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Mwanza (TPA), Kanda ya Ziwa Victoria, Abraham Msina wakati alipokagua ujenzi wa bandari hiyo katikati ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi Mamlaka ya Bandari TPA Bw. Leonard Magomba.
Injinia wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Mwanza (TPA), Kanda ya Ziwa Victoria, Abraham Msina akiongozana na baadhi ya waandishi wa habari na wakandarasi wa bandari ya Nyamirembe Chato wakati alipofanya ukaguzi katika eneo la mradi jana.
Mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa bandari ya Nyamirembe Chato , Injinia Anderson Mbogowe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Injinia wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Mwanza (TPA), Kanda ya Ziwa Victoria, Abraham Msina akifafanua jambo kwa waandishi wa habari waliotembelea mradi huo.
Sehemu ya ujenzi wa gati hilo ukiendelea.
Injinia wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Mwanza (TPA), Kanda ya Ziwa Victoria, Abraham Msina akionyesha mawe yanayotumika katika ujenzi wa gati katika Bandari ya Nymirembe Chato sambamba na ujenzi wa majengo ya abiria na jengo la kuhifadhia mizigo.
……………………………………………………………..
Injinia wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Mwanza (TPA), Kanda ya Ziwa Victoria, Abraham Msina amesema ya Nyamirembe, Wilaya ya Chato mkoani Geita, inatarajiwa kukamilika Agosti 23, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari bandarini hapo jana, Abraham Msina alisema mradi huo unaendelea na uko katika hatua ya asilimia 40 utekelezaji.
Mradi wa ujenzi huo utagharimu Sh. bilioni 4.1 ambazo ni fedha za serikali, unajengwa na Mkandarasi wa ndani ambaye ni Kampuni ya VJ Mistry, kutoka Bukoba mkoani Kagera.
Alisema sehemu ya kazi iliyobakia ni kumalizia ujenzi wa gati, jengo la abiria, jengo la mizigo, chumba cha mashine ya umeme, vyoo na chumba cha walinzi.
Msina alisema bandari hiyo itakapoanza kazi itachochea biashara kati ya nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na nchi jirani.
“Katika gati hili, meli ziliacha kuja miaka minane iliyopita kwa sababu kampuni iliyokuwa inaleta meli hizo ilisitisha huduma hiyo kwa sababu zao wenyewe lakini Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) wameurudisha mradi huu,” alisema.
Naye mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi huo, Injinia Anderson Mbogowe alisema hadi jana mradi huo umefikia asilimia 47 na wanatarajia kukamilisha kazi hiyo Julai na kisha kuukabidhi kwa serikali Agosti mwaka huu.