Na Mwandishi Wetu.
KOCHA mpya wa Simba SC, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck ameahidi kuipa klabu hiyo mafanikio makubwa kisoka kwa kushinda nyumbani na kufanya vyema kwenye michuano ya Afrika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Vandenbroeck alisema kwamba amevutiwa na Simba SC kutokana na mashabiki wake weng.
“Kilichonivutia Simba cha kwanza ni uwingi wa mashabiki. Ni jambo la kufurahisha kuona mashabiki 60,000 wakikushangilia inakupa hisia za kipekee,” amesema Vanderbroeck na kuongeza; “Lengo la kwanza ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu. Nataka kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, nataka kucheza mashindano ya CAF. Nataka Simba iwe kwenye hatua kubwa na kupata matokeo mazuri,” amesema.

“Lengo la kwanza ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu. Nataka kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, nataka kucheza mashindano ya CAF. Nataka Simba iwe kwenye hatua kubwa na kupata matokeo mazuri,
Vanderbroeck, mwenye umri wa miaka 40 amekuja kujiunga na Simba SC baada ya kuachana na timu ya taifa ya Zambia na atakuwa anasaidiwa na kiungo na Nahodha wa zamani wa klabu hyo Suleiman Matola.